WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUPUUZA TAARIFA KUHUSU AFYA YA RAIS MAGUFURI


Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa mitandaoni juu ya Afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Waziri Mkuu amesema hayo hii leo March 12 Mkoani Njombe mara baada ya kushiriki swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Wilaya  ya Njombe ambapo amewataka watanzania kuwa watulivu kwani Rais Magufuli yupo salama na anaendelea na majukumu yake.

 

Aidha amewataka watanzania kuendelea kuliombea Taifa, huku viongozi  wakitakiwa kukemea roho za chuki na kuhimiza upendo miongoni mwa watanzania.

 


Post a Comment

0 Comments