Na Isaac Aron, Kigoma
Waziri wa elimu
Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ameagiza kuvuliwa madaraka kwa mkuu
wa chuo cha ufundi stadi veta mkoani Kigoma kutokana na kushindwa kusimamia
vyema ujenzi wa chuo cha Veta Wilayani Buhigwe mkoani humo.
Ndalichako alitoa
maagizo hayo katika ziara yake ya kutembelea ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi
Veta katika wiaya za Uvinza,Kasulu na Buhigwe vinavyojengwa chini ya mpango wa
serikali wa kujenga vyuo 25 nchi nzima kwa gharama ya shilingi billion 40
katika awamu ya kwanza.
Ujenzi wa chuo cha
ufundi stadi Veta wilayani Buhigwe ambao unajengwa na chuo cha veta mkoani
kigoma unatarajiwa kugharimu shilingi billion 1.6 kwa ujenzi wa majengo 17
ambayo yanatakiwa kukamilika mwisho mwa mwezi june mwaka huu.
Waziri wa elimu Prof
Joyce Ndakichako anatembelea mradi huo na kuonyesha kutiridhishwa na ujenzi
wake kutokana na kujengwa chini ya kiwango cha serikali na kumlazimu kutoa
maagizo kwa mkurugenzi wa Veta nchini.
Mkurugenzi mkuu wa
Veta Dkt Pancras Bujulu alieleza kupokea maagizo hayo na kufanyia marekebisho
katika mradi huo ili kufikia mwezi june wananchi waanze kupata huduma katika
chuo hicho.
Baadhi ya wakazi
kutoka wiliya za Buhigwe Uvinza na Kasulu waliishukuru serikali kwa ujenzi wa
vyuo hivyo utakaosaidia jamii zao kujiendeleza kiuchumi kupitia elimu za stadi
ya maisha watakayopata katika vyuo hivyo.
Katika hatua nyingine
Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako alitoa maelekezo kwa vyuo vyote vya veta
ambavyo vimepewa dhama ya ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi kuhakikisha
wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati ifikapo mwezi june mwaka huu.
0 Comments