Mkurugenzi wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka, |
Na
Mwandishi Wetu,
Magonjwa ya mlipuko hasa
kipindupindu imetajwa kuwa tishio kwa maendeleo ya ustawi wa jamii na uchumi wa
mataifa mengi Barani Afrika hasa yaliyopo Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la
Sahara, Tanzania ikiwamo.
Aidha, pamoja na magonjwa hayo,
nchi zilizopo katika ukanda huo zinakabiliwa pia na majanga mengine ya kiasili
kama vile ukame, mafuriko na migogoro jambo ambalo linapelekea magonjwa ya
mlipuko kuathili zaidi wananchi wa maeneo hayo
Nchi ya Tanzania kwa muda mrefu sasa imekuwa ikiendelea kupambana
na magonjwa ya mlipuko huku magonjwa ambayo yamekuwa yakisumbua wananchi katika
maeneo mbalimbali nchini yakiwa ni pamoja na Kipindupindu
Wakati mapambano hayo yakiendelea Imelezwa kuwa Tanzania imefikia
hali ya kupungua kwa kasi ya magonjwa ya mlipuko hususan kipindupindu hapa
nchini ndani ya miaka 5.
Hayo yalielezwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) ambapo limesema, kupungua huko kumetokana na
usimamiaji mzuri wa sheria na kanuni za mazingira.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa NEMC, Dk. Samuel
Gwamaka, alisema kuwa utoaji wa elimu hasa katika kipindi cha awamu ya tano ni
moja ya sababu, pia amewapongeza Watanzania kwa kuweka mazingira
safi na salama bila shuruti.
Dk. Gwamaka aliongeza kwamba chanzo kikubwa cha magonjwa ya
milipuko nchini ni utiririshaji wa maji taka katika maeneo ya makazi ya watu
pamoja na maji ya kemikali zenye sumu kutoka viwandani ambayo huelekezwa katika
mito na makazi ya watu.
Hata hivyo Dkt Gwamaka alisema kuwa kutokana na mwitiko
chanya wa wananchi, NEMC imeunda kikosi kazi cha dharura ambacho kinafanya kazi
saa 24 huku kazi yake ikiwa ni kuhakikisha changamoto za kimazingira
zinashughulikiwa kwa wakati.
0 Comments