Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF umezindua mpango wa utoaji
bima ya afya kwa waandishi wa habari nchini baada ya UTPC kufanya mazungumzo na
NHIF kukubali waandishi kuwa na kifurushi chao maalum.
Akifungua mpango huo, mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela
amewataka waandishi wa habari kuacha ubahili na kulipia fedha hizo ili kuwa na
uhakika wa matibabu wanapougua.
Nae Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo ameushukuru mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
NHIF kwa kujali afya za waandishi wa habari huku akiwashukuru pia waandishi wa
habari nchini nzima kwa kuomba wawetengewe kifurushi chao maalumu.
“Asante Press club zote nchini ambazo wakati maafisa wa NHIF
wanapita kuhamasisha mikoani waandishi walipaza sauti kuanzia Mtwara hadi
Kagera kuomba kifurushi maalum na UTPC kufanya coordination na hatimaye sasa
mpango umeanza rasmi” alisema Rais wa UTPC
Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo |
Rais Deogratius amebainisha kuwa hadi sasa mkoa wa Kigoma licha
ya kuwa na wanachama wachache ndo inaongoza kwa waandishi kuwa na bima ya afya.
Ameongeza kuwa wanachama wa press clubs nchini wanakaribia 1800
lakini mpango huu umezinduliwa ukiwa na
wandishi 80 pekee
Hata hivyo Rais Deogratius ametoa wito kwa kwa waandishi wote
hata wale wasio wanachama wa press club kujiunga
na mpango huo kupitia press club katika mikoa yao.
0 Comments