WANANCHI BUHIGWE WAMPONGEZA MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO


 Na Mwajabu Hoza, Kigoma

WAKAZI wa kijiji cha Kasumo wilaya Buhigwe mkoani Kigoma eneo ambalo amezaliwa Mkamu wa rais Mteule Dkt Philip Mpango wamempongeza kwa hatua aliyofikia lakini pia kumuomba kuendeleza juhudi zake katika  kulitumikia Taifa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Ndugu,mjirani na wakazi wa kijiji hicho wameeleza kupokea kwa furaha nyadhifa aliyopata na kueleza hatua hiyo ni kutokana na jitihada zake alizokuwa akizifanya  tangu alipokuwa kijijini hapo.             

Ilikuwa siku ya Jumapili ya Julai 14 mwaka 1957 katika kijiji cha Kasumo wilaya Buhigwe mkoani Kigoma siku ambayo alizaliwa kijana ambaye leo hii ni Mkamu wa rais mteule wa awamu ya sita katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu zake wanamuelezea kuwa upole,uadilifu na uchapakazi imekuwa ni hulka yake tangu alipokuwa kijana mdogo na hatua aliyofikia kwa sasa ni matunda ya jitihada zake za kila siku kuhakikisha anawatumikia wa Tanzania.

Genviev Tegera ambaye ni  dada yake na Dkt Philip Mpango pamoja na Antony Mpango mtoto wa mdogo wake Dkt Philip Mpango wameeleza kufurahishwa na hatua aliyofikia ndugu yao ambaye wanaamini kuwa jukumu alilopewa atalifanya kwa ukamilifu na kwa umakini wa hali ya juu.

Mjirani pamoja na Wakazi wa kijii hicho wanaeleza kujivunia na hatua aliyofikia kwani wana Imani na Dkt Philip Mpango kwa uwezo wake wa kulitumikia Taifa lakini pia kuhakikisha jamii anayotokea inaendelea kuimarika kiuchumi kutokana na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara iliyopo kwenye kijiji anachotokea.

Mwaka 1968 mpaka 1970 katika shule ya msingi Muyama alimaliza elimu yake ya msingi, Nikaona nifike shuleni hapo walau kuona darasa alilosomea na kuzungumza na waalimu ambao Stella Shayo mkuu wa shule ya msingi Muyama anasema wataendelea kumuenzi kwa kuinua ufaulu na kutoa neno kwake juu ya uboreshaji wa miundo mbinu shuleni hapo ambapo majengo yamechakaa lakini pia walimu kukosa nyumba za  kuishi .

Yasini Kuhunguru ni mwalimu mstaafu na aliyesoma na Dkt Philip Mpango anaeleza “Tangu awali dkt. Mpango alikuwa na akili sana darasani na alikuwa akifanya vizuri katika somo la hisabati na kingereza na alikuwa wanafunzi mtiifu na mwenye weledi wa hali ya juu” alisema

Ni nderemo na Vifijo katika eneo la sokoni kwenye kijiji cha Kasumo kijiji ambacho amezaliwa makamu wa Raisi Mteule Dkt Philipo Mpango wakieleza kujivunia kwa mmoja wa wanakijiji mwenzao kushika nafasi ya juu na muhimu nchini nafasi ambayo haijawahi tokea kwa wakazi wa mkoa wa kigoma tangu kupatikana kwa uhuru.

Post a Comment

0 Comments