ONGEZEKO LA MAJI ZIWA TANGANYIKA LAWAATHIRI WAKAZI MKOANI KIGOMA

 


Adela Madyane, Kigoma

Wananchi wanaoishi mwambao mwa ziwa Tanganyika pamoja na ofisi mbali mbali zilizopo pembezoni mwa ziwa Tanganyika eneo la Kibiri Mkoani Kigoma wamekubwa na  athari za kimazingira kutokana na ongezeko la maji katika ziwa hilo tangu April mwaka 2021.

Kwa mujibu wa Muhandisi  kutoka bodi ya maji Bonde la ziwa Tanganyika Respicious Mshogozi alisema chanzo cha athali hiyo ni maji kushuka toka mwaka 1974 na kuanza kupanda mwaka 2006 ambapo takwimu ya chini kusomwa ilikuwa772.85 ambayo  ni sawa na ongezeko la nusu mita   kutoka kwenye usawa wa ziwa toka mwaka 2006.

Mshogozi alisema maji yalianza kuongezeka na  hadi kufikia April mwaka 2012 kina cha maji kilipanda na kusoma776.42 kutoka wa ziwani .

Takwimu hizo zimeendelea kubaki kuwa 776.47 kwa mwezi May 202. Wastani wa ziwa ni sawa na 772.35 hivyo kuleta ongezeko la sentimeta 4.12 kutoka  wastani wake.

Mshogozi ameongeza kuwa maji yataanza kupungua kunzia mwishoni mwa mwezi wa 6 kuelekeza wa 7, na yapungua zaidi kuanzia mwezi wa 9 na wa 10,na yataanza kuongezeka zaidi kuanzia Novemba 2021 ambapo mvua zinatarajia kuanza kunyesha.

David Manyama Kaimu Mkurugenzi wa bonde la maji  Ziwa Tanganyika, alisema kuwa maziwa yakijaa hupungua taratibu, na zipo sasababu kuu mbili za asili zinazopunguza maji ambazo ni maji kuvukizwa, mvuke kupanda angani na maji kutoka  kwenye njia yake ya asili.

“maji ya ziwa Tanganyika yanatoka  kwenda ziwa Atlantiki kupitia mto Lukuga uliopo Kalemi nchini Kongo, mto Lukuga hupeleka maji yake katika mto mwingine mkubwa zaidi ambao huo huingiza maji mto Kongo na kisha kuingia kwenye bahari ya Atlantiki ” Alisema Manyama.

Sababu nyingine ndogo za kupunguza maji ziwani kwa kiasi kidogo ni matumizi ya shughuli za kibinadamu zinazohusisha kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya nyumbani.

Vipo vyanzo na njia mbalimbali zinazoogeza maji ziwani zikiwemo mvua, mitoinayotiririsha maji ziwani, na maji chini ya ardhi, kuna mikondo inayoingiza maji ziwani, uwiaono wa maji unaoingia na kutoka ziwani ndio unaosabababisha maji kupungua au kuongezeka.

Maji yanayotoka yakiwa mengi kuliko yanayoingia husababisha kupungua kwa maji, huku maji yanayoingia yakiwa mengi kuliko yanayotoka maji huongezeka kulingana na mabadiliko ndani ya mwaka mmoja ambapo maji hujaa na kupungua.

“ tumeshuhudia ongezeko la maji kuongezeka toka mwaka 2006 lakini zaidi kwa miaka ya 2019 mpaka sasa, hii inamanisha kuwa maji yanayotoka ni machache kuliko maji yanayoingia” alieleza Manyama.

Maji kuongezeka huchukua miaka 15-30 na kupungua huchukua pia miaka 15-30, hivyo kuna mzunguko wa miaka 60 ya maji kuongezeka na kupungua na kitendo hicho  hutendeka taratibu, ushuhuda wake ni mdogo kwa kuwa tabia hiyo haijitokezi kwa kasi.

Hata hivyo vitendo hivyo hufanyika kwa maziwa yote duniani na hasa maziwa  yaliyopo Africa, na kwa kipindi hiki maziwa yote ya Afrika yamejaa, hata yale yaliyokuwa kwenye hatari ya kukauka huku akitoa mfano wa ziwa Chad, Turkana pamoja na Natron.

Bakari  Mwichande kaimu mkuu wa kampasi ya Kigoma katika chuo cha Elimu ya afunzo ya uvuvi (FETA) akielezea namna gani ogezeko la maji limeathiri mazao ya ziwani ikiwemo samaki na dagaa.

Mwichande alisema ongezeko la maji ni faida kwa samaki na dagaa kwa kuwa maji yakiongezeka wanapata maeneo mapya ya kuishi na vilevile huweza kuzaliana  kwa wingi.

“Maeneo ambayo hayajafuni kwa na maji yanakuwa na nyasi, miti, mizoga na uchafu tofauti tofauti mbao hutumika kama chakula kwa samaki na vingine vikioza hutoa  vimelea  ambavyo vinatumika na mime iliyopo ndani ya maji kutengeneza chakula pamoja na oxgen” alisema Mwichande.

Akizungumzia upatikanaji wa sumu zinazotokana na shughuli za kibinadamu ambazo kutokana na ongezeko la maji alisema hakuna dawa ya kutibu samaki waliopo ziwani kwani madawa yanayoingia ziwani hubadiilika na kuwa chakula kwa baadhi ya viumbe walioko majini na hivyo kutoleta mdhara yoyote.

Alisema kuwa  kutokana na muingiliano wa maji kutoka vyanzo tofauti tofauti vinavyofanya sumu inayosambazwa mpaka inafika ziwani inakuwa haina nguvu tena kama ambavyo ingaingia bila kukumbanan a vyanzo vingine vya maji.

Akifafanua  namna ambavyo samaki na viumbe wengine wa majini wanavyoweza kupata madhara kutokana na kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kufuatia ongezeko la maji alisema, viumbe wanaopatikana katika ziwa, mito, au hata bahari, huishi kwenye maeneo ambayo temperature, pressure, chemical, light, food na oxgen vinaendana na viumbe husika.

Mwichande alisema hali hiyo ikitokea kiumbe akaingia katika maeneo ambayo hajayazoea hujitahidi kurithi mazingira na akishindwa basi hutafuta namna ya kurudi alipotoka.

Kwa upande wa mamlaka ya hali ya hewa, Meneja wa kituo Kikuu cha utabiri Mamlaka ya hali ya hewa   Tanzania  Samweli Mbuya, alisema wamekuwa wakitoa utabiri wa hali halisi ilivyo ikiwemo mvua, joto na upepo, na tabiri hizi zimekuwa zikiambatana na tahadhari hasa mifumo ya utabiri inapoimarika na kudsababisha mvua nyingi.

Alisema mvua zinaweza kuwa za muda mfupi au za muda mrefu (za msimu) kwa maana mvua kuwa juu ya kiwango cha kawaida taarifa zimekua zikitolewa kwa uhakika na usahihi kabisa.

Akizungumzia changamoto hiyo wananchi, Rashid Omary alisema wamepata hasara za kichumi kutokana na soko kujaa  maji  hali mabayo inakwamisha shughuli za kibiashara kufanyika vizur.

Pamoja na kukwama kwa shughuli za kiuchumi, miundombinu ya barabara imethirika ambapo daraja la linalounganisha kata ya Gungu na Kibirizi lipo katika hatari ya kubomoka na ubomokaji wake utaleta chanagmoto za usafirishaji.

                                                                                                                                      Muhandisi kutoka NEMC na kaimu mwenyekiti wa bodi ya bonde la ziwa Tanganyika Delfrina Igulu, amezishauri mamlaka na wanachi  kufanya shughuli za kijamii mita 60 kutoka kwenye    vyanzo vyote vya maji na kuseam kuwa jamii zilizopo pembezoni mwa vyazno vya maji zichukue hatua stahiki kwaajili ya usala wake.

Benjamini Dotto Meneja NEMC kanda ya magharibi alitoa wito kwa wawekezaji kufanya tathmini za athari za mazingira lengo kupata ushauri kutoka kwa wataalamu mbalimbali kabla ya kuchukua hatua yoyote ya ujenzi  kwani mchakato wa tathmini ya athari utasaidia kupunguza changamoto za kimazingira na za kijamii kwa uwekezaji endelevu.

“Wananchi tutekeleze matakwa ya kisheria ya usimamizi wa maji namba 11 ya mwaka 2009 inayotutaka tujenge au tufanye shughuli zetu nje ya mita 60”.

Mwisho. 

 

Post a Comment

0 Comments