WADAU NCHINI WATAKIWA KUTOA MAONI KUHUSU MITAALA



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 

Waziri wa Elimu nchini,  Profesa Joyce Ndalichako amesema kumekuwa na kilio kikubwa kuhusu mitaala ya elimu nchini hivyo ipo haja ya kukusanya maoni ya wadau kuhusu suala hilo.

 

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo Ijumaa Juni 18, 2021 wakati wa mkutano  wa kupokea maoni ya wadau wa elimu kuhusu uboreshaji wa mitaala ya elimu nchini nakuongeza kuwa Kilio kuhusu mitaala kimekuwa kikubwa kuanzia bungeni, mitandaoni na hata wanaoleta maoni yao bungeni.

 

“Kilio kimekuwa kikubwa kuanzia bungeni, mitandaoni na hata wanaoleta maoni yao bungeni hatimaye leo tumekutana wadau toeni maoni.”“Tunataka mitaala ikajibu kiu ya Watanzania na hili lina maana kubwa kufanyika chiniya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema

 

Aidha Waziri Ndalichakoi ameongeza kuwa serikali  inataka mitaala ikajibu kiu ya Watanzania huku jambo hilo likiwa na maana kubwa kufanyika chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Hata hivyo amesema kuwa mabadiliko ya mitaala yanapaswa kuendana na sera ya taifa ambayo inahusu viwanda kwani kwa sasa ni awamu ya sita.

 

 


Post a Comment

0 Comments