Na Diana Rubanguka, Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philipo Mpango, ameiagiza
idara ya uhamiaji Mkoa wa kigoma kufanya kazi kwa weledi wanapofuatilia
wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufata taratibu na sheria za nchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Viwanja
vya Mwanga Community Centre mkoani hapo akiwa katika wizara yake ya kwanza
tangu achaguliwe kuwa makamu wa Rais wa Tanzania.
Aidha Dkt Mpango aliitaka idala ya uhamiaji kuwa ifanye kazi kwa umakini wakati wa kuwatambua wananchi wanaishi mkoa wa Kigoma ambao siyo raia wa Tanzania badala ya kuwabambikizia kesi ya uhamiaji wananchi wa kigoma ambao ni wazawa na raia wa Kigoma.
Kufuatia hali hiyo, amewaagiza kukaa pamoja na wabunge ili
kujadili namna bora ya kuhakikisha wale ambao si raia na wanaishi
nchini kinyume na taratibu za nchi wanachukuliwa hatua stahiki na si kumsumbua
kila mwananchi kwa kigezo cha kuzaliwa Kigoma.
“kigoma nzima tumegeuzwa wahamiaji, Mimi mwenyewe nilishabatizwa jina
mitandaoni naitwa mrundi na wakati Burundi nimefika mara moja nilipoagizwa na
raisi wetu kwenye kumbukizi ya aliyekuwa raisi wa Burundi hayati Nkurunzinza,
tusihukumiwe kwakuwa tunaishi Kigoma na tupo karibu na Mipakani" alisema Mpango
“Kumekuwa na kasumba ya kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wa mkoa wa Kigoma
kwa kuwabambikizia kesi za uhamiaji hali inayowafanya wanachi kuishi bila amani
katika mkoa na nchi wanayozaliwa na kushindwa kutekeleza majukumu yao ya
kiutafutaji kwa kuhofia kukamatwa| aliongeza Dr Mpango.
Katika ziara hiyo amezindua jengo la ofisi za takwimu mkoa wa kigoma ambao
amesema kuwa sensa inayotarajia kufanyika 2022 ni kwa manufaa ya jamii na
kusema kuwa kujua idadi ya watu itasaidia katika kupanga miradi ya
maendeleo na kuitambua mahitaji yao kwaajili ya utekelezaji wa huduma
wanazostahili.
Hata hivyo kufuatia wimbi la mgonjwa wa Uviko (Covid 19) Dkt Mpango ametoa wito
kwa jamii kuendelea kufuata taratibu za kujikinga zinazotolewa na wataalamu wa
afya kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.
“korona ipo, niwaombe ndugu zangu tusifanya mzaha na ugonjwa huu kwani upo na unaua, tuendelee kunawa mikono kwa maji tililika kama tulivyoelekezwa, kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari nyingine" alieleza Dkt Mpango
Akitoa takwimu za ugonjwa huo amesema, mpaka sasa tuna wagonjwa
18 katika mkoa wa Kigoma huku Tanzania nzima wagonjwa wakiwa 471, kwa
takwimu hizi mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa 10 yenye wagonjwa wengi.
0 Comments