Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kuanzisha
vitalu vya kuzalisha miche ya Zabibu ili kuwawezesha wakulima kupata mbegu kwa
uhakika.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumanne (Julai 06, 2021) alipokua akizungumza na
wadau wa uendelezaji wa zao la Zabibu Jijini Dodoma, ambapo amesema vyama vya
ushirika wa kilimo cha zao hilo kuanzisha pia vitalu hivyo ili kuwawezesha
wananchama kupata mbegu bora.
Pia
Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kupitia
kituo chake cha Makutupora iimarishe utafiti wa zao hilo, ili kupata miche bora
na yenye tija na kuifikisha kwa wakulima,
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kupitia kampeni ya kuendeleza zao hilo,
Serikali itasimamia kuhakikisha zao la Zabibu linayolimwa nchini linakuwa na
ubora wa hali ya juu, lengo likiwa ni kupata soko la uhakika ndani na nje ya
nchi.
Naye, Naibu
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kwa sasa Wizara ya Kilimo imeanza
usajili wa wakulima wa zabibu ili waweze kuwatambua na kuwafikia kwa urahisi.
Amesema
mbali na usajili wa wakulima, pia wizara hiyo imeanza majadiliano ya kuanzisha
mfuko wa maendeleo ya zao hilo ambao utachangiwa na wenye viwanda na wakulima.
Wakulima
wa zao hilo wameiomba Serikali iwasaidie katika upatikanaji wa pembejeo, mikopo
pamoja elimu ya namna bora ya kulima zao hilo ili waweze kuongeza tija katika
uzalishaji wao.
0 Comments