Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya lipuli, Tabora Tarehe Julai 3, 2021.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora
WAZIRI wa Kilimo, Prof
Adolf Mkenda amewaonya baadhi ya viongozi wenye tabia ya kuingialia Vyama vya
Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) huku akiwataka kuacha tabia hiyo mara
moja.
Aidha, amesema ushirika
sio idara ya serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama idara kwakuwa mamlaka yake
ina mipaka na hakuna kiongozi anayetakiwa kuingilia matumizi ya fedha wala
kuzipangoa matumizi.
Waziri Mkenda ametoa
agizo hilo (Jumamosi, Julai 3,
2021) kwenye kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja
vya lipuli, Tabora, ambapo alisema kwa kiasi kikubwa serikali imepambana
kurejesha mali mbalimbali za ushirika zilizokuwa zimeibiwa kupitia ushirika.
”Tumepambana sana na
wabadhilifu kwenye ushirika na kurejesha mali mbalimbali zilizoibiwa kupitia
ushirika hivyo kurudisha imani ya wanaushirika, na mali zao haziwezi kufanyiwa
ubadhirifu wa aina yoyote.
Tutaendelea kusimamia
ushirika kuhakikisha kwamba unaendelezwa kwa weledi, uwajibikaji na uwazi ili
watu wengi wakubali kujiunga na ushirika kwa sababu unasaidia sana kunyanyua
hali zao za kimaisha kwa kuwa ni hiari kujiunga hakuna
kulazimishwa,”alisema.
Alieleza kuwa ushirika ni
hiari na msingi wa kwanza duniani na kwamba ni kweli ushirika sio idara ya
serikali hivyo hauwezi kuongozwa kama IDARA YA SERIKALI KWAKUWA mamlaka yake
kwenye ushirika yana mipaka yake.
”Na hili ni muhimu kwa
sababu kuna mahali ametokea kiongozi mmoja kaingia kwenye AMCOS anatoa amri toa
shilingi milioni ishirini na tano hapa peleka kule, hatuna mamlaka hayo,
ushirika ni hiyari ya wanaushirika
”Na hapaswi kupelekesha
wana ushirika wanapaswa kujisikia kwamba ushirika ni mali yao, wasimame kidete,
wasimamie shughuli zao bila kuingiliwa kinyume na taratibu
zinazokubalika,”alisema.
Alisisitiza anasema hilo
kwa sababu kuanzia Waziri wa kilimo (yeye), Mrajisi wa ushirika, wote lazima
wajue mpaka upi wa kwao au si wao
”Mpaka sasa tunakwenda
vizuri ukiacha hilo tukio mtu kwenda kutoa amri chukua hela za ushirika kutoka
eneo moja kupeleka eneo ambalo ushirika huo hauhusiki nalo kwenda kujenga
shule,
”shule ni jambo zuri
lakini hakuna mamlaka ya kiongozi yoyote kwenda kuingia kwenye ushirika
kuingilia fedha zao kuzipangia matumizi hayo yatafanywa na wanaushirika wenyewe
,”alisema.
0 Comments