Na Mwandishi Wetu, Kibondo
Baadhi ya wakulima wilayani Kibondo mkoani
kigoma wameiomba serikali kusisitiza uwajibikaji kwa maafisa ugani kuwatembelea
wakulima na kuwapa elimu juu ya magonjwa yanayoshambulia mazao yao ili kulima
kilimo chenye Tija na chenye kuleta maendeleo kwa wakulima.
Wakizungumza kwa
nyakati Tofauti na blog hii walisema wamekuwa wakitumia Mbinu za kienyeji
kutambua magonjwa yanayoshambulia mazao yao , na kwamba wakati mwingine
mazao yamekuwa yakiharibiwa na wadudu kutokana na wakulima kukosa elimu ya
kilimo.
Afsa Ugani wilaya ya
Kibondo Albert Fatakanwa alisema changamoto inayoikabili wilaya ya
hiyo ni uhaba wa maafisa Ugani kulinganishwa na kata za wilaya hiyo , na kwamba
wamekuwa wakitumia baadhi ya wakulima viongozi kwenye vijiji kuwaelimisha
wakulima wenzao ili kukabilina na changamoto hiyo.
0 Comments