Na Mwajabu Hoza ,
Kigoma
TAKRIBANI asilimia 72
ya watoto wa kike wamefanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo ukatili wa wa
kihisia, kimwili na kingono na asilimia 71 ya watoto wa kiume nao wakiwa
wamepitia ukatili kama huo kwa mkoa wa Kigoma.
Katika takwimu hizo
asilimia 60 ya watoto wamefanyiwa ukatili wa kihisia ikiwemo kutukanwa,
kudhalilishwa kwa maneno mabaya na kutishwa na ukatili ambao umeanza kupatiwa
Baraka katika jamii na kuonekana ni jambo la kawaida.
Kwa mujibu wa tafiti
zilizofanywa mkoa wa Kigoma katika kipindi cha mwaka 2011 watoto wa
kike wamekuwa waadhirika wa matukio ya ukatili ambapo kati ya watoto wa kike
100 wenye umri chini ya miaka 18 asilimia 30 wamefanyiwa vitendo vya ukatili
huku kati ya watoto saba wenye umri chini ya miaka saba mmoja kati yao
amefanyiwa ukatili.
Akizungumza na
wananchi wa kata ya Murufiti wilaya ya Kasulu Mji mkuu wa Mkoa Kamishna wa
polisi Thobias Andengenye amesema matukio hayo yamekuwa yakifanywa na watu wa
karibu ikiwemo wajomba, baba, baba wadogo, shangazi, na majirani na ukatili
umemgusa kila mtu hivyo jamii inatakiwa kushikamana kwa pamoja kupinga vitendo
hivyo.
“Mtoto akibakwa
anaweza kutibiwa michubuko lakini maumivu yaliyopo ndani ya moyo hayawezi
kutibiwa na daktari na hivyo tunatengeneza watoto ambao wataishi na maumivu
miaka yote ya maisha yao.”
Amesema hatuwezi kuwa
na jamii ambayo kila mtoto amefanyiwa ukatili hali ambayo inahatarisha usalama
wa Taifa kwa kuendelea kutengeneza watoto ambao watakuwa wakiishi na visasi
ndani ya mioyo yao hivyo ni vyema wazazi kujenga tabia ya kuzungumza nao ,
kuwalinda na kuwadhamini watoto kwa kujua changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.
Aidha ameonya tabia ya
baadhi ya jamii wakuozesha watoto wao wakiwa katika umri mdogo lakini pia
kuacha tabia ya kuwatumikisha watotokatika shughuli za uzalishaji mali na
kuwafanya kitegauchumi cha familia na kuhatarisha usalama wa maisha yao mzazi
anajukumu la kumpatia mtoto wake elimu bora na malezi mazuri.
Merania Samweli ni
mzazi ambaye ameeleza kuwa ukatili unaofanywa na wanaume kwa wakezao ikiwemo
vipigo mara kadhaa umekuwa ukiadhiri malezi ya watoto ndani ya familia na
hhivyo kusababisha watoto kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao.
0 Comments