MFAHAMU DIWANI ALIYEDUMU MADARAKANI KWA ZAIDI YA MIAKA 35

 

Mzee Alhaji Kassim Nyamkunga

Adela Madyane -Kigoma

Uadilifu, ukweli, ukakamavu na kupenda watu, nguzo pekee zilizomfanya Alhaji Kassim Nyamkunga kudumu katika udiwani kwa miaka 36 sawa na vipindi saba vya uongozi kuanzia mwaka 1985 mpaka 2021.

Nyamkunga alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha mwamgongo, akiwa ni mtoto wa 6 kati ya watoto 12 wa mzee Kassim Nyamkunga huku elimu yake ikiwa darasa la 7 na elimu ya dini kiislamu

Diwani huyu aliyedumu katika nyadhifa zake kwa muda mrefu pa bila kuvunja imani ya wananchi wake ana jumla ya wake 4, watoto 21, 16 wakiwa hai na 5 waliofariki, na wajukuu zaidi ya 45.

Shughukli zake  kuu kabla ya kuingia katika siasa ilikuwa ni uvuvi pamoja na kilimo cha mchikichi alizozifanya kwa miaka zaidi ya 20, na baadae kuwaachia vijana kwa kuwapatia ajira, katika kipindi hicho alimiliki mitumbwi 17 na zaidi ya ekali 10 za michikikichi, baadae aligawa mitumbwi 10 kwa ndugu zake ili wapunguze utegemezi nayeye kubakiwa na mitumbwi 7 pekee.

Mzee Alhaji Kassim Nyamkunga akiwa na mke wake.

Safari ya siasa

Mnamo mwaka 1968 hisia za kuingia katika siasa ziliibuliwa na ujio wa Riasi wa kwanza wa Tanzania hayati Julias Kambarage Nyerere aliyetembelea kijiji cha Mwamgongo siku ya Jumnne terehe17/09/1968 akiwa na lengo la kufanya shughuli zake za kiserikali ndipo alipougusa moyo wa Nyamkunga na kumfanya kuingia katika siasa rasmi.

“Baada ya ujio wa Mwalimu, niliigia katika umoja wa vijana chipukizi TANU, na huko baada ya kuwa mwanachama wa muda mrefu, nikiwa na miaka 33   nilifanikiwa kushika nafasi ya ukatibu waTawi kata ya  Mwangongo na kuongoza vijana kwa miaka 3”alieza Nyamkunga

Akiendelea na harakati za uongozi, akiwa na miaka 35, Nyamkunga  aliaminiwa na wanachanawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukabithiwa kijiti cha kuwaongoza wanachama hao kwa muda wa miaka 5 akiwa kama mwenyekiti huku silaha zake kuu zikiwa ukweli, ukarimu, juhudi, kazi na kupenda watu bila ubaguzi wowote.

 

Akiwa na umri wa miaka 41 mnamo mwaka 1985 alichaguliwa rasmi na wananchi wa kata ya Mwamgongo kwaajili ya kuwaongoza kama diwani wa kata hiyo yenye vijiji vitatu vya Mwamgongo, Mugamba na Kiziba

Nyamkunga alieleza kuwa, alidumu katika udiwani kama diwani wa kawaida kwa muda wa miaka 2 kabla hajagombea umakamu wa mwenyekiti katika baraza la madiwani ambapo alipata na kudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 2 mingine.

Historia yake haikuishia hapo kwani alizidi kushika nyadhifa tofauti tofauti na kutengeneza historia ya kuwa kiongozi aliyedumu kwa muda mrefu ukilinganisha na viongozi wenzake .

 “Baada ya kushika nyadhifa ya makamu mwenyekiti, niligombea nfasi ya mwenyekiti CCM kata ya Mwamgongo nikapata na nimewahudumia wananchi katika nyadhifa hii kwa kipindi cha miaka 10, wakati huo huo niligombea nafasi  ya  kuwa mweyekiti wa baraza la madiwani la halmashauri nikapata na nikaongoza kwa miaka 15” Alifafanua Nyamkunga.

“Sikuishia hapo, nilitamani kufanyua mambo mazuri zaidi, na ndipo nilipogombea nafasi ya kuwa ALAT, na Mungu alinisaidia nikashinda pia, kwenye nyadhifa hii nilikuwa  nawaongoza wenyeviti kutoka halmashauri 6 za mkoa wa Kigoma, na nilisimama katika nafasi hii kwa miaka 10” Alielelzea zaidi .

Sambamba na uongozi wa serikali, Nyamkunga pia ni kiongozi katika dini ya kiislamu ambapo mpaka sasa ni mweyekiti wa BAKWATA wa kata ya Mwamgongo.

Alisema “Elimu ya dini imenisaidia sana kuwa mkweli na muadilifu kwa watu ninaowaongoza, sina ubinafsi, mimi ni mtu wa watu na ninajitioa kikalifu kutimiza ahadi nilizoziweka kwa wananchi ninaowangoza” Alimalizia kwa msisitizo.

Mafanikio.

Kwa miaka yote ambayo amekuwa madarakani, Nyamkunga amefanikiwa kutekeleza miradi yote aliyoahidi kwa kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya, miundombinu ya barabara  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, pamoja na ujenzi wa shule ya msingi na sekondari

Kwa upande ujenzi wa kituo cha afya  Nyamkunga alieleza “ Tulikuwa tunapata changamoto sana ya kupata huduma za afya, hasa kwa wajawazito na wagonjwa waliozidiwa, ilitughrimu kutumia usafiri wa boti kutoka Mwamgongo mpaka Kigoma mjini kwaajili ya  huduma za afya ambapo huchukua takriba masaa 3 mpaka 4, na baadhi wagonjwa wengi walipoteza maisha” Alieleza.

“Kutokana na changamoto za usafiri kuwa nyingi, mnamo mwaka 2008 mimi na wananchi wangu tuliamua kuchonga barabara kwa mikono kwa muda wa miezi 4 ambapo tulifanikiwa kutengeneza kilometer 18 kutoka Chankere  mpaka Mwamgongo, na baadae serikali iliingilia kati na kuongeza kilometa 20 kutoka Mwamgongo mpaka Mwandiga.” Alifafanua zaidi.

Kwa furaha Nyamkunga alisema kuwa barara hiyo ndio kitu pekee anachojivunia nacho zaidi , na barabar hiyo inaitwa jina la Nyamkunga, ilizinduliwa na waziri mkuu Mizengo Pinda.

Katika sekta ya elimu, kata hiyo imefanikiwa kujenga shule 3 za sekondari ambapo mbili zimekamilika na moja imefika kwenye renta na shule moja ya msingi na hivyo kuwafanya watoto kuhudhuria masomo yao bila changamoto yotote.

Matarajio yake.

Nyamkunga alieleza kuwa, anatarajia kuwaona vijana wengi wakijitokeza kugombea nyadhifa za uongozi na kwamba anatamani watakaoshinda wawaongoze wananchi katika misingi ya haki.

“Siri kubwa ya uongozi bora ni kuwa mwadilifu na muamiaminifu, mchapa kazi na muwazi, mimi nilizijenga nguzo hizo kwa wanachi wangu,vivyo hivyo natamani watakaokuja baada yangu, hasa vijana wafanye vizuri zaidi yangu” Alieleza.

Diwani Mke katika familia yake

Sambamba na yeye kuwa Diwani kwa kipindi chote hicho mkewe wa 4  Hidaya Swalehe Kimpwi,naye ni diwani wa viti maalumu kata ya Mwamgongo aliyedumu katika nafasi hiyo kwa  vipindi vitano kuanzia mwaka 1994 kabla ya mabadiliko ya taratibu za kiuchaguzi ya kuungunisha uchaguzi wa wabunge, madiwani na raisi mpaka sasa.

Hidaya Swalehe, ni mtoto wa 2 kwa mama yake na mtoto 10 kwa baba yake, alizaliwa mwaka 1968 na elimu  yake ni darasa la 7, ni mama wa watoto 5 na aliolewa mwaka 1996 kwa mzee Yasin Nyamkunga.

Alisema “Nilijiunga kuwa mwanachama wa CCM mwaka 1989 na nikateuliwa kuwa katibu wa kijiji na katibu wa Tawi la CCM Matyazo kwa muda wa miezi 5, baadae nikahamishiwa Uvinza  nikiwa katibu wa Tawi la CCM Uvinza ambapo nilihudumu kwa miaka 5pia”.

“Manamo mwaka 1994, nilipitishwa na chama kuwa  diwani wa viti maalumu na baadae nilifanikiwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake kuanzia mwaka 1996 kwa miaka 15 sasa” Alifafanua zaidi. 

Akielezea mahusiano yake na wake wenzie 3, alisema kuwa toka ameolewa anaishi vizuri na wake wenzie.

“Ukewenza ni mwanaume, mwanaume akiwa katili atawachanganya wanawake na wao wataishi kwa kuangaliana vibaya ila mwanaume akijielewa wanawake watasimama vizuri kwaajili ya malezi na ustawi wa familia kwa ujumla”.Alisisitiza Swalehe

Baadhi ya wananchi wakizungumiza juu ya uongozi wa Alhaji Kassim Nyamkunga wake, na sababu za wao kuendelea kumchagua kwa kipindi chote hiki.

Wakiongea katika nyakati tofauti, wakazi wa kijiji cha Mwamgongo ambapo ndipo makazi ya diwani huyu yalipo walisema kuwa Nyamkunga amekuwa akiwatumikia wananchi kwa kufuata ushauri wa wananchi na si kwa matakwa yako binafsi.

Juma Ahmad Kimalarungu alisema Nyamkunga amekuwa akiongoza utawala wake kwa kufuata sheria na na taratibu za uongozi, sambamba na hilo amekuwa na upendo mno kwa wananchi wake.

 Alisema “Diwani wetu ana haki ya kudumu katika uongozi kwa kipindi kirefu kwa kuwa anajali utu wa mtu, ana upendo kwa wananchi wake na kamwe hajawahi kuwatelekeza, kwa mfano,  anajuhudi za kutafuta maendeleo ya wananchi wake na pale wanapokuwa na matatizo ya kijamaa anawasaidia, anakwenda hospitalini na mahakamni pia. Alifafanua kwa undani

Naye mjumbe wa halmashauri ya kijiji Pili Issa Nyota anaeleza kuwa diwani huyu ni diwani ambaye anategemewa kwenye shughuli za maendeleo na shughuli za kila siku, anahakikisha kile alichokiahidi kwenye kampeni kinakuwa cha kweli, anapambana mpaka anakitekeleza.

“Diwani wetu huyu anajali sana, habagui wanachi wake ki chama, anawaongoza wote katika usawa “, "Tunaendelaea kumpa nafasi kwakuwa ni muwazi, hana uongozi wa uficho, anaongoza vizuri, anajali na afya zetu, hata kwenye ujenzi wa barabara  alikaa na wananchi wake kufyeka majani kwa miezi 4, kutoka Chankere mpaka Mwamgongo" Akijisikia kuongoza tena tupo nyuma yake tutamfanyia kampeni za nje na ndani.  Alieleza kwa shauku.

Naye Yasin Mohamed mwemyekiti wa kitongoji aliyepita wa Chama cha Wananchi CUF alisema kuwa Nyamkunga ni kiongozi mzuri japo anatakiwa kumalizia barabara ya Buhagara mpaka Mwamgongo ili kuendelea kupunguza changamoto ya usafiri iliyopo.

 “Kuna kipindi ziwani hakuingiliki, unakuta wimbi ni kubwa na ukilazmisha kuingia majini unaweza kuzamisha boti, inabidi diwani wetu aendelee na haratakati za kumalizia barabara hiyo, tupate usafiri wa nchi kavu wa kuaminika.” Na ni matumaini yangu kuwa serikali itampatia sapot ya kumalizia barabara ili tuondokane kabisa na changamoto za usafiri. Alieleza Mohamed.

Post a Comment

0 Comments