JAMII YATAKIWA KUACHA TABIA YA KUMALIZA KESI ZA UKATILI KIENYEJI

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya

Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya ameitaka jamii kuacha tabia ya kumaliza kesi za ukatili kienyeji na kubainisha kuwa  mila na desturi kandamizi zinachangia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Mmuya amesema mashirika, wadau na taasisi zisizo za kiserikali zishirikiane na Serikali katika kuondoa mila na desturi Kandamizi ambazo  zinachangia  matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii

Ameyasema hayo leo kwenye ziara yake mkoani Shinyanga wakati alipo itembelea shule ya Agape inayomilikiwa na shirika la Agape mkoani humo linalotetea haki za wanawake na watoto

Aidha katika ziara yake amekutana na kamati ya ulinzi na usalama na wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga pamoja na wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA)

Mmuya ameiomba  jamii kuacha tabia ya kumaliza kesi za ukatili kienyeji huku  akivishauri vyombo vya dola ikiwemo Polisi na Mahakama kukaa na kujadili namna ya kuondoa changamoto ya ucheleweshaji wa kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto

“Mila na desturi kandamizi katika maeneo mengi ndiyo inachangia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Mila hizi tunaziendekeza sisi kwa kufanya vikao ngazi ya familia na kumaliza kesi za ukatili kienyeji. Tunalipana fedha na mali na kumaliza kesi za matukio badala ya kupeleka kesi kwenye vyombo vya sheria huku vyombo vya sheria navyo vikilaumiwa kuchelewesha maamuzi matokeo yake ushahidi unapotea na matukio yanaendelea kutokea”,amesema Mmuya

 

Post a Comment

0 Comments