CHANGAMOTO ZA UVUVI ZIWA TANGANYIKA ZAWAKUTANISHA WADAU WA UVUVI

 


Happiness Tesha, Kigoma.

Wadau wa uvuvi wamekutana mjini Kigoma,kujadili na kuthibitisha matokeo ya utafiti wa mnyororo wa thamani wa dagaa,  samaki wa ziwa Tanganyika na changamoto wanazokabiliana nazo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na uvuvi , Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji, Dkt Nazael Madalla amesema mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika nchi 12 za Afrika, umefanya utafiti huo ili kuweza kuangalia zaidi changamoto zinazowakabili wadau hao.

Amesema ili waweze kuwa na maamuzi sahihi ya kisera na kisheria lazima waelewe uvuvi unafanyaje na changamoto ziko wapi ili maamuzi yote yanapofanyika yaende kutatua changamoto hizo katika namna sahihi.

" Mradi wa FISH4ACP ni wa kipindi cha miaka mitano ambapo umeanza mwaka 2020 na kuhusisha nchi 12 na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya na wizara ya maendeleo ya mashirikiano ya uchumi ya Ujerumani na kutekelezwa na Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Kimataifa (FAO),"amesema Madalla.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dkt Ismael Kimirei amesema waliweza kuwafikia watu 500 katika utafiti wao na kwamba katika utafiti huo waliweza kubaini biashara ya mazao ya uvuvi inafanywa na watu wa hali ya chini hivyo.

Amesema utafiti huo itasaidia kuwapa matokeo chanya yakayowasaidia kuwaboreshea mazingira rafiki wafanyabiasha na wavuvi katika ziwa Tanganyika.

Mtaam wa Uvuvi kutoka Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO), Hashim Muumin amesema wanaenda kufanyia kazi maoni ya wadau walioyakusanya lengo kuwaongeza thamani katika sekta ya uvuvi.

 

Post a Comment

0 Comments