HIFADHI YA GOMBE KUTOA ELIMU YA CHANJO YA UVICO 19 KWA JAMII INAYOWAZUNGUKA

Pichani ni wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigoma baada ya elimu ya chanjo ya UVICO 19.


Diana Rubanguka, Kigoma. 

Hifadhi ya Taifa Gombe iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma imeahidi kuendelea kutoa elimu ya Chanjo ya Uvico -19 lengo kuhakikisha watumishi wake na jamii unayowazunguka wanachanjwa ili kuwakinga wanyama waliopo hifadhi hiyo.

Hayo yameelezwa na mkuu wa kitengo utafiti wanyama polo katika Hifadhi ya Gombe chini ya Taasisi ya Jane Goodall Dkt. Anthony Collins baada ya wataalam kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambapo alisema wanaunga mkono  juhudi hizo ili kuwakinga Sokwe na Nyani kwa kuwa wanashabihiana na binadamu hivyo ni rahis kuambikizwa.

Dkt. Collins alisema, kulingana na maisha ya kifamilia wanayoishi katika hifadhi hiyo kupata chanjo itasaidia kumkinga Sokwe kwa kuwa ni kiumbe chenye asili ya binadamu.

"Sokwe ni kiumbe chenye asili kama binadamu tofauti ni Sokwe ana ubungo mdogo na hawezi kuongea, lakin kamwili na ki DNA na kiasili wapo kama binadamu, lila ugongwa anaopata binadamu na Sokwe anapata" alisema Dkt . Collins.

ikiwa ugonjwa huu ni hatari kwa binadamu ni hatari pia kwa Sokwe na Nyani hivyo ni jukumu lao kutunza afya za wanyama hao kama wanavyotunza afya zao kwa kuwa  wanaweza kufa wote hali ambayo nitaleta hasara kwa Taifa.

"japo tuna mtindo wa karantini kwa watumishi kila wanapotoka likizo, lengo letu ni kuhahakikisha hawana ugonjwa wowote ambao wanaweza kuwaambukiza wanyama" aliongeza Dkt. Collins.

Kaimu  mhifadhi mkuu  wa hifadhi hiyo Sailasi Mbise ambaye pia ni mhifadhi mkuu mazingira alisema, ni jambo jema kwa kuwa watumishi wameweka kuwa n uelewa kuhusu maswali yaliyokua yanawatatiza kuhusu chanjo.

Aidha Mbise alisema, chanjo hiyo ni muhimu sana kwa hifadhi kwa kuwa Mtumishi mwenye afya njema ndiye mwenye uwezo wa kufanya kazi na utendaji kazi bora ni chanzo ya mapato kwa Taifa.

"Ikumbukwe wakati wa mlipuko wa virus vya ugonjwa huo tulipoteza mapato ya watalii na hoteli, sasa tumepata huduma hii tutahamasisha lengo tuwakinge wafanyakazi na wanyama" Alisema Mbise.

 

 


Post a Comment

0 Comments