JAMII YATAKIWA KUPATA CHANJO YA UVIKO 19 NA KUACHANA NA UPOTOSHAJI

Wafanyabiashara wa soko la Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji wakiendelea na shughuri zao za kila siku

Na Emmanuel Senny, Kigoma

Wakati serikali ikiendelea na zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi wote Tanzania, Wakazi wa Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiasa jamii kujitokeza kupata chanjo badala ya kuendekeza dhana potofu na uzushi usio na uhakiki kuhusu chanjo hiyo. 

Wakizungumza na blog hii katika soko la Kibirizi wakazi hao akiwemo Ally Bilali Kigogo, Juma Masodi na Ngema Mstafa wamesema kwasasa kila mtu anatakiwa kujali maisha yake na kujikinga na ugonjwa wa Corona ambao umekuwa tishio katika mataifa mengi duniani hivyo chanjo ni muhimu kwa kila mtu bila kuhofia upotoshaji wa baadhi ya watu.

“Ushauri ni kuchanja kwa sababu Corona ni janga la dunia nzima, hakuna haja ya kusikiliza maneno ya kupotosha kwasababu huwezi jua anaepotosha huenda yeye amechanja ila anataka tu kuwapotosha wengine, lazima watu tukubali kuchanja kwasababu serikali imeshaona ili kuokoa wananchi wake ni vyema kutoa chanjo kwa kila mtu na aliyechanja ni bora zaidi kuliko ambaye hakuchanja” walisema

Aidha Wananchi hao  waliiomba sekta ya afya kuongeza chanjo katika vitu vya afya na Zahanati ili watu wanaokwenda kupata huduma hiyo wasipate usumbufu  wa kurudi mara mbilimbili huku pia wakiwaomba wahudumu wa afya wanaosimamia zoezi la kusamba chanjo mitaani wafikie kila eneo ili watu wote wapate huduma hiyo

“Nilienda kufatilia chanjo katika kituo cha afya ya Kikunku lakini nikaambiwa zimeisha hivyo ni vyema serikali ikaongeza chanjo ili kuokoa maisha ya watu, kwa upande wangu sijapata chanjo ila nikikutana na watoa huduma nitachanga hivyo basi wajitahidi kutembelea maneo yote ili sisi wote tupate huduma” waliongeza

Kwa mujibu wa Mratibu wa Chanjo kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa Henry Kisinda alisema dozi 53,508 za UVIKO 19 zimepokelewa ikiwa ni awamu ya pili ambazo zitagawanywa katika halmashauri nane za mkoa na kila halmashauri inapata dozi 6,608


Post a Comment

0 Comments