MBINU ZA UHAMASISHAJI CHANJO YA UVIKO 19 ZA ZAA MATUNDA

 

Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Mahembe kilichopo kata ya Mahembe Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mkoani humo Daktari Elius Juma (katikati) akizungmza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Diana Rubanguka, Kigoma

Imeelezwa Kuwa mbinu mbali mbali za uhamasishaji  wa kuchanjwa chanjo ya COVID -19 imekua chachu ya mwananchi kujitokeza kwa mwingi kuchanjwa chanjo hiyo.

Hayo yameelezwa na mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Mahembe kilichopo kata ya Mahembe Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mkoani humo Daktari Elius Juma.

Dkt. Juma alisema, baada ya uongozi ngazi Mkoa kuanzisha kampeni ya chanjo kwa njia ya Mkoba, walibuni njia ya kutumia Wazee maarufu, viongozi wa kijiji pamoja na Kombola yaani spika ambayo inawafikia watu wengi kwa wakati mmoja.

"Tumebuni njia ya kutumia Wazee maarufu kwa kuwa wanasikilizwa na watu wengi, viongozi wa kijiji pia wanaushawishi kwa wananchi wao kuanzia mwenyekiti, mtendaji kata hadi vitongoji kupitia wao lakini pia Kombola likitangaza watu wengi wanasikia na wamejitokeza sana kuchanjwa" alisema 

Mratibu wa chanjo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Nasibu Ally alisema, walipokea chanjo ya covid -19 August 03,2021 na kuanzia kampeni August 05,  2021 katika vituo vya Bitale, matyazo na zahanati ya Simbo.

 Klinic ya Mkoba pamoja na matangazo ya elimu yamesaidia kuongeza idadi ya waliochanjwa siku hadi Siku ambapo hadi kufikia 14 Octoba zaidi ya nusu ya dozing zilizotolewa zilikua zimekwisha tumika.

Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina ya watumishi wa afya kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi  ya jamii huku akikili spika ya matangazo kuwa chachu katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Hassan Mnyonge muuza chipsi katika kijiji cha Mahembe alisema, kwa sasa kati ya watu 50 wa kijiji hicho  45 wamechanjwa na hadi sasa wanaendelea kuchanjwa na kusema kuwa hakuna aliyechanjwa na kupata madhara yoyote

Post a Comment

0 Comments