RAIS SAMIA: SERIKALI ITAENDELEA KUENZI NDOTO ZA HAYATI MWL. NYERERE

 








Na Mwandishi Wetu, Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu  Hassan, amesema serikali itaendelea kuzienzi ndoto, na Fikra chanya za Maendeleo za aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Manufaa ya Kizazi cha Sasa na Kijacho.

Rais Samia ametoa kauli hiyo akiwa Chato Mkoani Geita wakati wa Sherehe ya Kitaifa ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambapo pia ilikuwa ni Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa.

Sanjari na hayo amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru, zinamanufaa makubwa kwa Taifa la Tanzania,  kwani ni chachu ya Viongozi wa Serikali kuwa waaminifu wakati wa kutekeleza miradi ya Maendeleo.

Awali Msimamizi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akisoma lisara ya Utii, Ruteni Josephine Paul Mwambashi amesema mbio za Mwenge zimekutana na upungufu Mkubwa wa Miradi ya Maendeleo kwa baadhi ya Halmashauri hapa nchini.

 

Post a Comment

0 Comments