WANAHABARI WATAKIWA KUIBUA CHANGAMOTO KWA MASLAHI YA JAMII NA TAIFA

 

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma, aliyekaa ni Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Kigoma KGPC.

Na Mwajabu Hoza , Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye ametoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini kutumia taaluma waliyonayo katika kuibua changamoto zilizopo katika Jamii kwa lengo la mamlaka husika kuchukua hatua za kiutekelezaji kwa maslahi ya jamii na Taifa

Andengenye ameyasema hayo wakati wa Mdahalo wa kujadili Uhuru wa Kujieleza, Maadili ya Uandishi wa Habari na Kumuenzi Baba Wa Taifa Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere mdahalo ambao umehusisha  wanahabari, taasisi za umma na wadau wa habari.

Amesema waandishi wanajukumu kubwa la kuelimisha umma hivyo watumie vyema fursa waliyonayo kwa kuzingatia maadili yao na bila upendeleo wowote katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiuandishi.

Amesema Tasnia ya habari ni taaluma pekee inayoaminiwa na jamii kwa haraka na kwa muda mfupi hivyo ni vyema kutumia taaluma kuelimisha jamii kwa usahihi kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.


“ Nawasisitiza andikeni habari , kosoeni , fichueni mapungufu kwa lengo la kurekebishana na hiyo ndio kazi yenu kama muhimili wa nne wa nchi na kupitia ukosoaji huo utasaidia taasisi za serikali na watu binasfi kuweza kurudi katika mstari na wala lengo lenu sio kwenda kuchukua nafasi zao” amesema

Raisi wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Deogratius Nsokolo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma KGPC amesema Vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa na ni jukumu la kila mwandishi kupaza sauti kwa niaba ya wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye akiwa katika picha ya pamoja na waandshi wa habari mkoani Kigoma.

Amesema katika kumuenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwa kumuenzi kwa kufanya kazi kikamilifu kwa kuyaishi maono yake kwa kusaidia kulinda amani kuandika kwa wedi kwa kuzingatia taaluma, maadili kuwa wa kweli na kuheshimu wengine.

“Tujue kwamba tuko kama wananchi wengine tunaongozwa na katiba pamoja na sheria mbalimbali” amesema

Aidha Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa haabri walioshiriki katika mdahalo huo Richard Katunka amesema waandishi wanapaswa kuyaishi yale yaliyokusudiwa katika Mdahalo huo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa Jamii na Taifa kupitia taaluma yao.

Post a Comment

0 Comments