Mmoja wa wananchi wilayani Kasulu akipata chanjo baada ya watoa huduma kuwafikia |
Na Deogratius Nsokolo
Wananchi katika kata za nyachenda na asante nyerere katika halmashauri ya wilaya ya kasulu mkoani kigoma, wamesema hatua ya wataalam wa afya kutembea katika vitongoji na vijiji kuhamasisha na kutoa chanjo ya ugonjwa wa uviko 19 inasaidia watu wengi na hasa wazee wasio na uwezo wa kutembea umbali mrefu kupata huduma ya chanjo ya corona.
Wamesema hatua ya wahudumu wa afya kuwafuata wananchi imeondoa hofu na kufanya idadi kubwa ya watu kujitokeza kupata elimu na kuamua kuchanja ambapo wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuhakikisha chanjo zinakuwepo katika maeneo yote ya kutolea huduma vijijini.
Mtoa huduma akitoa elimu kuhusu chanjo ya Uvico 19 kwa baadhi ya wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma |
Kwa upande wake mratibu wa chanjo
katika halmashauri ya wilaya ya kasulu elia thomas amesema watoa
huduma katika halmashauri hiyo wameweza kuvifikia vijiji vyote ikiwa ni pamoja
na maeneo muhimu kama masoko na minada ili kutoa huduma ambapo amewahimiza
wananchi kuendelea kujitokeza kupokea chanjo ya uviko 19 ili kujikinga na
ugonjwa huo.
0 Comments