WANANCHI KIGOMA WAJITOKEZA KUPATA CHANJO YA UVIKO 19 BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA

 


Na Diana Rubanguka, Kigoma

Wananchi wa kata ya Mwandiga ambao wamejitokeza kupata chanjo ya UVICO - 19 wamesema kutojali itikadi za vyama vya siasa imekua chachu ya wananchi kujitokeza kuchanja.

Hayo yameelezwa mmoja wa wananchi waliochanjwa Boazi Chuma aliyekua msaidizi wa Mkuu wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe ambapo alisema kuwa wameamua kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chanjo haina chama. 

Chuma alisema, pamoja na kuwa kata ya Mwandiga imekuwa na historia upinzani wa kisiasa lakini katika suala la chanjo wameamua kuwa mstari wa mbele kuchanja kwa kuwa suala la Corona linagusa maisha ya watu halipaswi kuingiliwa na masuala ya kisiasa.

"Nilikua mtu wa nne kuchanja, habari za kuweka mambo ya uchama tumeweka pembeni na tunaendelea kuhamasishana ili kuhakikisha wote tunachanjwa" alisema chuma.

Akizungumzia suala la mafanikio ya chanjo Shabani Hemedi ambaye pia ni shuhuda wa alisema namna ya tawala zilivyo na kusema sababu kubwa ya kuweka uchama pembeni imetokana na ambavyo awali wamewahi kupata hasara kwa kusukia vitu vinavyoletwa na serikali ambayo ni chama tawala.

"Siku za nyuma tumewahi kupata hasara kwa kukataa chanjo ya homa ya ini ambayo leo hii inalipiwa pesa ili kuipata na yote hayo ya kutoipata chanjo hiyo yalichangiwa na sababu za uchama" alieleza Hemedi.

Hata hivyo alisema kuwa, watu wa ukanda huo wana tabia ya kuacha siasa baada ya uchaguzi ambapo alisema baada ya uchaguzi wanaungana na chama kilichoshinda kuwa kitu kimoja kwa maendeleo ya nchi na wananchi.

Afisa afya Zahanati ya mwandiga Costancia Petro alisema chanjo za awali walizowahi kuchanjwa Wazee imekua chachu kwa jamii kujitokeza zaidi kuchanjwa ambapo alisema Wazee hao wamesema toka awali wamekuwa wakichanjwa na hakuna chanjo iliyowahi kuleta madhara kwa jamii.

Alisema Wazee hao walisema, ugonjwa wa surua ulisumbua sana watu na baada ya chanjo ya surua kupatikana na watu kuchanjwa ugonjwa huo ulipotea katika jamii na kutoa wito kwa jamii uzidi kujitokeza kuchanjwa kwa kuwa ni neema ya pekee kupata chanjo ya bure

 

 

Post a Comment

0 Comments