Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Zaidi ya Shilingi Bilioni 63 Zimepokelewa Katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa kunusuru kaya Masikini Mkoani Kigoma, ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 53 kati ya hizo tayari zimewafikia walengwa hadi kufikia Mwezi March 2021.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma Msafiri Nzunuri, alieleza hayo wakati akisoma Tarifaa ya Sekta ya Maendeleo ya Jamii, katika Kikao kazi kilichowakutanisha Viongozi Mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Christopher Kadio.
Wakati huo huo baadhi ya Wazee kutoka Baraza la Wazee Mkoani hapa , waliiomba Serikali kuongeza Juhudi za kuweka Mazingira wezeshi zaidi kwa kundi hilo, ili wasiendelee kuwa tegemezi kwa Watoto wao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk John Jingu, alilithibitishia kundi
la Wazee hapa nchini kuwa Serikali itaendelea kuboresha Mazingira rafiki kwao,
huku Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Christopher Kadio akisema Wazee
wanamchango Mkubwa Kwa Maendeleo Ya Taifa.
0 Comments