WANANCHI MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA ZAHANATI



Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Wananchi wa Mtaa wa Buronge Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamepongeza hatua ya Serikali kukamilisha ujenzi wa zahanati katika mtaa huo hali itakayosaidia kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya.

Wananchi hao wamesema Kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilazimika kufuata huduma za afya katika kituo Cha afya Gungu, lakini Kwa Sasa huduma zinazotolewa ngazi ya zahani watazipata karibu.

Kwa upande wake mtendaji wa kata ya kibilizi Bw Richard Magai Amesema zahanati hiyo imejengwa Kwa nguvu za wananchi Kwa kushilikiana na serikali huku akieleza kuwa wananchi wa mtaa wa buronge, bushabani na Ntovye watanufaika zaidi na mradi huo.

Awali Mganga mfawidhi wa kituo hicho Missana Milson Amesema watalaamu wote wamejipanga kutoa huduma Bora Kwa wananchi ili kuokoa maisha ya watu na kuondoa adha kwa wananchi ya kusafiri umbali mrefu.

 


Post a Comment

0 Comments