Na Emmanuel Matinde,
Kigoma
Zaidi ya wananchi elfu kumi wa
Kijiji cha Mwayaya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, wanatarajia
kupata huduma ya maji safi na salama baada ya mradi wa maji wa chanzo cha mto
Kivuruga unaojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2.3 chini ya ufadhili wa
Shirika la Enabel kukamilika.
Hayo yalielezwa na Eng. Respicius
Kahamba, Mhandisi wa Maji kutoka Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Vijijini RUWASA Wilaya ya Buhigwe, ambaye amesema kwa sasa ujenzi wa mradi huo
umefikia asilimia zaidi ya 90%.
Alisema mradi huo Pamoja na miradi
mingine inayotekelezwa katika Wilaya ya Buhigwe yote kwa Pamoja
ikigharimu zaidi ya Shilingi Bilioni tisa, itaongeza upatikanaji wa maji safi
na salama kwa wananchi.
Wakati hayo yakiendelea Bodi ya
Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika, ilibainisha mikakati ya kukabiliana na tishio
la uharibifu wa chanzo cha mradi wa maji wa Kijiji cha Mwayaya ili kuhakikisha
unakuwa endelevu.
Wakati huo huo mradi wa maji
wa Kijiji cha Mnanila katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ambao unajengwa
kwa fedha za UVIKO 19 Shilingi Milioni 400 umeanza kutoa maji.
Wilaya ya Buhigwe ina jumla ya
vijiji 44 ambapo ambapo kwa sasa asilimia 72 ya vijiji hivyo ndiyo hupata maji
safi na salama.
0 Comments