Wananchi
Mkoani Kigoma wameshauriwa kuwa na desturi ya kufanya mazoezi na kupima afya
zao mara kwa mara ili kuweza kuondokana na magonjwa nyemelezi.
Wito
huo ulitolewa na Afisa Mahusiano kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Bw. Timoth
Fasha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ufanyaji wa Mazoezi uliopewa jina la
Wellness Day ambayo imefanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika.
Bw.Timoth
alisema kuwa wafanyakazi wamekuwa hawapati muda wa kufanya mazoezi kutokana na
majukumu walionayo ofisini na hivyo Benki ya CRDB wameamua kutenga siku ya
kuwakutanisha wafanyakazi wao ili kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao.
Naye
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa siku ya Wellness day, Bw. Ngassa Maxmiliani
akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Kigoma Bi. Esther Mahawe alisema hakuna
shughuli yoyote ambayo inaweza kufanyika bila kuwa na afya njema hivyo mazoezi
muhimu kwa kila mwanadamu.
Akizungumza
kwa niaba ya Wafanyakazi wa matawi yote ya Benki ya CRDB Mkoani Kigoma, Meneja
wa CRDB tawi la Kigoma Bw. Arrison Andrew alisema wamefurahishwa na mtakakati
wa banki yao kuwa na program hiyo kwani kutofanya mazoezi muda mwingi unaweza
kukumbwa na magonjwa.
Uzinduzi
wa Kampeni hiyo ya Wellness Day umeenda sambamba na zoezi kupima afya zao kwa
wafanyakazi na wananchi waliojitokeza uwanjani hapo.
0 Comments