MATUKIO YA UKATILI KWA WATOTO YAZIDI KUSHAMIRI KATIKA JAMII



Mwajabu Hoza , Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo Ya Jamii Jinsia Wanawake Na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima amesema  ukatili kwa watoto umezidi na kufikia matukio elfu 11, 499 kwa mwaka 2021 ukuachilia mbali kubakwa na kulawitiwa lakini pia kuchapwa , kutukanwa na kufinywa  imekuwa kawaida kwa jamii kuwafanyia watoto wao mambo ambayo yanaadhiri ukuaji wa ubongo wa mtoto na hivyo jamii kuhitaji elimu ya umuhimu wa sayansi ya malezi, makuzi na maendeleo  ya awali ya mtoto.

Ametoa kauli hiyo wakati  akifungua  mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (Science of ECD) ambayo yamefanyika  jijini Dodoma kwa kipindi cha siku sita.

Waziri Gwajima amesema ukatili wanaofanyiwa watoto ni kutokana na jamii kukosa elimu sahihi ya makuzi na malezi mazuri ya watoto hali inayochangia watoto wengi ukuaji wao kutokuwa timilifu kutokana na changamoto zinazotokana na jamii inayowazunguka hivyo ni matarajio ya serikali kwa wale waliopata mafunzo ya( SECD ) kutekeleza vyema wajibu wao katika kuelimisha jamii kupitia makongamano, midahalo, matqmasha na maandamano ya amani yatakayochangia mabadiliko ya makubwa katika jamii jinsi ya kuwapa watoto ilinzi na usalama pamoja na lishe bora.

"Jamii itambue kuwa kipindi cha umri kuanzia miaka 0 hadi 8 ni kipindi muhimu sana cha ukuaji wa ubongo wa mtoto na ni wakati mzuri wa kumpatia mtoto malezi mazuri ili tuweze kutengeneza Taifa lenye watu wenye uelewa mzuri na viongozi wa zuri wenye tija kwa Taifa katika nyanja za  kimaendeleo na kiuchumi , hivyo ni jukumu la kila mmoja kumpatia mtoto ulinzi mzuri " amesema .

Amesema ili kufikia lengo la mpango wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto, Serikali itawekeza ili mpango huu uwe na tija na vituo vilivyopo katika mikoa viweze kuwa na mafanikio katika jamii  kupitia wataalamu waliopata elimu ya SECD na kupitia elimu waliyopata tuweze  kutengeneza ngome imara katika ukanda wa Afrika kupitia program mbalimbali ikiwemo Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto (PJT MMMAM).

Lakini pia Serikali kwa washirikiana wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari  Serikali inatarajia mapinduzi makubwa kwenye Tasnia ya habari kitaifa na kimataifa  katika kuhakikisha kuwa jamii inapata uelewa mzuri na taarifa sahihi kuhusu Sayansi ya malezi na makuzi ya watoto. 

Kwa upande   Mkurugenzi wa  Shirika la CiC, Craig Ferla amesema, Program hiyo Jumuishi inachochea utekelezaji wa mipango mingi katika  sekta za ECD na ili kufikia lengo ni washiriki wote wa kimtandao wanaohusika kwenye masuala ya ECD pamoja na kushirikiana na serikali kupitia taasisi zote za kisekta ili kuwa na nguvu ya pamoja na kushurikiana kupitia rasilimali zilizopo kuleta tija kwa watoto na kuwa na utekelezaji wa kiwango cha juu.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari Victor Maleko kutoka Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) akimwakilisha  Mkurugenzi mtendaji amesema waandishi wa habari nchini wameendelea kuhabarisha umma  kuhusu malezi, makuzi  na maendeleo ya awali  mtoto  kupitia vyombo mblimbali vya habari ambapo tangu kuzinduliwa kwa mpango MMMAM katika kipindi cha miezi 6 tu zaidi ya habari 450 zimesharipotiwa habari pamoja na vipindi.

" Tunaahidi mpaka program inakamilika wadau wengi watakuwa wanafahamu nini maana ya ECD na kutakuwa na uwekezaji mkubwa katika kuwatengeneza watoto wa Taifa hili ambao watakuwa na uwezo mkubwa wa kulijenga vyema Taifa lao, na tangu mwaka 2019 mradi huu wa ECD umeanza zaidi ya habari 1000 zimeripotiwa na tunaimani kasi hii itaendelea " amesema Victor    

Mafunzo hayo ya siku sita yanalenga kuongeza uelewa kwa sekta muhimu katika kuboresha huduma za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ambapo  washiriki  zaidi ya 70 wanapatiwa  mafunzo ya SECD ambayo yameandaliwa  kwa ushirikiano wa taasisi ya Children in Crossfire (CiC) TECDEN na UTPC  kwa makubaliano na Chuo Kikuu cha Aga Khan, ambapo  waandishi wa habari, viongozi wa Serikali, wizara za kisekta, maafisa maendeleo na  ustawi wa jamii mkoa na Asasi za Kiraia zimeshiriki.

 

 

 


Post a Comment

0 Comments