Na. Mwandishi Wetu, Bukoba Kagera.
Katibu mkuu wizara ya Afya Prof.Abel Makubi ametoa maagizo ya
kuongeza kasi ya uchunguzi katika mipaka ya nchi katika mapambano ya Ugonjwa wa
Ebola.
Prof.Makubi amebainisha hay oleo Septemba 29,2022 Wilayani
Bukoba Mkoani wakati akizungumza na watumishi hospitali ya rufaa ya
Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kufanya ziara maeneo ya mpakani Mtukula
kukagua hatua mbalimbali za serikali ambazo zimeshaanza kuchukuliwa katika
kukabiliana na Ebola ili usienee nchini baada ya kuripotiwa visa vya ugonjwa
huo nchi jirani ya Uganda hivi karibuni.
Aidha ,Prof.Makubi ameendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna
visa vya ebola hata kimoja vilivyoripotiwa hapa nchini.
“Kwa sababu kuna njia nyingi za kupita wananchi katika mipaka
nitoe maelekezo kuhakikisha kuongeza kasi ya uchunguzi katika mipaka tunaona
kuna mipaka mingi wananchi wanapita.
Kuhusu suala la Uelimishaji pamoja na kuweka vifaa muhimu vya
kupimo vya Ebola Prof.Makubi amesema wizara ya Afya imejipanga ambapo jopo la
wataalam wizara Afya Kwa kushirikiana na wataalam wa afya kutoka mikoa ya
mipakani ikiwemo Kagera wameendelelea kutoa elimu ambapo ameagiza kuongeza kasi
ya uelimishaji zaidi kwa njia ya vyombo vya habari na vipeperushi mbalimbali.
“Serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauenei
nchini na niwahakikishie watanzania hakuna Ebola Tanzania ,hatua ambazo
zimeshaanza kuchukuliwa ni pamoja kusambaza vifaa vya kupimia Ebola na
Ambulance “amesema.
Hivyo,Katibu mkuu huyo wa Wizara ya Afya amesisitiza
kuendelea kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.
Nao baadhi ya Wananchi mkoani Kagera akiwemo Fresta
Abdallah,Khadija Rasuli pamoja na Ale Thomas wameishukuru serikali kwa
kuendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na Ebola huku wakiomba
ukaguzi kuendelea kuimarishwa zaidi sehemu za mipaka.
0 Comments