Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliohitimu mafunzo ya mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) Manispaa ya Kigoma ujiji October 27, 2022. |
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) Manispaa ya Kigoma Ujiji. |
Vijana waliohitimu mafunzo ya mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) Manispaa ya Kigoma ujiji October 27, 2022 wakimsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe. |
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Vijana na watu wa rika zote nchini
wametakiwa kutoyachukulia poa mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) badala yake
wajitokeze kupata mafunzo hayo kwa kuwa yana faida nyingi lakini kubwa zaidi ni
kijana kuwa mzalendo kwa taifa lake.
Mara nyingi mtazamo wa jamii
umekuwa kwamba askari wa jeshi la akiba, au kama wanavyojulikana kwa jina la
Mgambo, ni watu wasumbufu na waonevu kwa raia kutokana na kutumiwa na mamlaka
za ngazi ya halmashauri katika shughuli mbalimbali, hasa pale wanapoonekana
kwenye uvunjaji wa vibanda vya biashara ya wamachinga.
Hata hivyo sivyo ilivyo, kama Chatta Emmanuel Kitanga na Hellen Mlondo
ambao ni wahitimu wa mafunzo ya mgambo walivyoeleza kuwa mafunzo ya mgambo
yanawafanya vijana kuwa wakakamavu na pia kuwa na utimamu wa akili.
“Hatupewi
mafunzo na vibaka ila tumepewa mafunzo na Askali wa jeshi la wananchi hivyo ni
mafunzo halali kabisa ambayo pia ni mlango wa fulsa kwetu” wamesema vijana hao.
Aidha askari wa jeshi la akiba
wamekuwa na faida nyingi kwa halmashauri; ni kutokana na umuhimu wao Mshauri wa
Mgambo Wilaya ya Kigoma Suleiman Mgeni Kassim, ameutaka uongozi wa halmashauri
kuwathamini.
“Tunaomba
ofisi hasa halmashauri kuwaongezea kipato vijana wa mgambo ili waweze
kukabiliana na maisha ili wasiingiwe na tama, ila pia kwa vijana mliohitimu hii
leo hakikisheni mnaendeleza mazoezi” amesema.
Akifunga mafunzo ya jeshi la akiba,
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Eshter Mahawe, amewataka wahitimu wa mafunzo
kutoyatumia mafunzo hayo kufanya ukatili majumbani mwao au katika jamii
wanayoishi.
“Msibadirishe
muelekeo, msitumie uzoefu mlioupata kwenda kuwatishia wazazi au ndugu zenu huko
nyumbani, kazi yenu ni kulinda raia na kuwa tayari muda wowote mtakapohitajika
katika kulinda mipaka ya nchi yetu” amesema Mahawe.
Mafunzo ya jeshi la akiba ni sera
ya ulinzi wa Taifa, na hutolewa kila mwaka na kila wilaya kote nchini.
0 Comments