UMOJA WA MATAIFA UMEOMBWA KUONGEZA JITIHADA KATIKA KILIMO NA AFYA

 

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Isaac Mwakisu wa kwanza kushoto na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR Ben Diallo wakiwa katika Maadhimisho ya miaka 77 ya mashirika ya umoja wa Mataifa.

Na Isaac Aron Isaac

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wameshukuru mchango wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Duniani UN katika miradi ya maendeleo na kuyaomba kuongeza jitihada katika sekta za kilimo na afya ambazo bado zinakabiliwa na changamoto.

Ikiwa leo ni Maadhimisho ya miaka 77 ya mashirika ya umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwakwe, hapa mkoani Kigoma yalianza kufanya  shughuli zake Mwaka 1996 baada ya wakimbizi kutoka nchi za Congo DRC na Burundi kuwasili mkoani hapa.

Wananchi ikiwemo Efrazia Zegeli na Zabibu Issa wanaeleza kwa miaka 26 ambayo mashirika hayo yamehuduma  yamewezesha miradi ya kimaendeleo lakini kwa sasa hali ya kilimo katika upatikanaji wa mbolea na Afya upande wa vifaa na vifaa tiba imeendelea kuwa changamoto.

Wanasema katika afya wananchi wanalazimika kununua baadhi ya vifaa hasa kwa wamama wajawazito hatua ambayo imekuwa ni changamoto kwa wale wenye hali duni hivyo wameomba mashirika hayo kutoa msaada wa vifaa hivyo katika vituo vya afya ambapo pia katika Kilimo wameiomba kutoa ruzuku ya mbolea licha ya serikali kupunguza bei kufikia mfuko mmoja kwa shilingi elfu 70.

Mkuu wa ofisi ya Shirika la Kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR Ben Diallo akizungumza katika maadhimisho hayo amesema Kupitia miradi kadhaa ambayo inaendelea kutekelezwa hapa Mkoani Kigoma ikiwemo Mradi wa pamoja wa Kigoma KJP ambao unatarajiwa kuanza hivi karibu kwa awamu ya pili unatajwa kugusa katika maeneo yote ambayo bado yanaonekana kuwa changamoto kwa wananchi mkoani humo.

Mkuu wa ofisi ya Shirika la Kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR Ben Diallo akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 77 ya mashirika ya umoja wa Mataifa. 


Akitoa salamu za serikali  katika maadhimisho ya siku ya mashirika ya umoja wa mataifa mkoani Kigoma Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu ameeleza kwa sasa mashirika hayo yameendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, biashara na kadhalika ambayo serikali inasimamia.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Isaac Mwakisu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya miaka 77 ya mashirika ya umoja wa Mataifa.

Aidha katika maadhimisho hayo ambayo yanaenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu limefanyika ikiwa ni sehemu ya kusaidia wale wenye mahitaji katika hospitali

 

Post a Comment

0 Comments