WAZEE WASIOJIWEZA KIGOMA WAOMBA KUBORESHEWA MAKAZI YAO


Na Mwajabu  Hoza, Kigoma

WAZEE wanaoishi kwenye makazi ya wazee Silabu kilichopo kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiomba serikali kuwapatia uzio katika eneo lao pamoja na kuwaboreshea nyumba zao ili kukabiliana na changamoto ya mvua na vibaka katika eneo hilo.

Wametoa kauli hiyo mara baada ya watumishi wa shirika la Posta mkoa wa Kigoma kuwatembelea na kuwapatia misaada mbalimbali ikiwa ni katika maadhimisho ya shirika la Posta duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Octoba 9 ya kila mwaka 

Ni tangu uhuru wazee wanaoishi katika makazi ya wazee wasio jiweza na familia zao zipatazo kaya 23 wamekuwa wakitaabika na mvua pamoja na wezi ambao wanachukua nguo na mazao yao kutokana na ukosefu wa uzio ikiwa ni kilio chao ni cha muda mrefu.

Wiston Bayinga  na Beatric Kachila ni baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi hayo ambao wanaeleza kuwa mazao wanayopanda ikiwemo matunda pamoja na nguo zao vimekuwa vikichukuliwa na vibaka wanaoingia katika makazi yao na kilio hicho kimekuwa hakitekelezeki licha ya kuomba mara kadhaa kwa serikali na wadau mbalimbali.

Afisa msaidizi kwenye makazi ya wazee Fredy David amesema kwenye kamazi hayo wazee wamekuwa wakiishi hapo lakini pia kuna watoto ambao nao walizaliwa katika makazi hayo nao ambapo jukumu la serikali ni kuwaunganisha na wadau mbalimbali kupata huduma za kielemu.

Ndagije Chobaliko ambaye ni Afisa mwandamizi kutoka shirika la Posta mkoa wa Kigoma amesema kila mwaka husherekea maadhimisho ya shirika hilo kwa kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo kutoa misaada katika makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na makazi ya wazee ambapo wametoa msaada wa Vyakula na sabuni kwa wazee hao.

Kaim meneja wa shirika la Posta mkoani Kigoma Juma Kahungenge amesema ukiachilia mbali hilo lakini pia ameeleza mafanikio ya shirika  katika kuifikia jamii kwa kuipatia huduma bora na za haraka kwa kuanzisha utuaji wa huduma kidigitali ikiwemo Duka mtandao na huduma hizo ni miongoni mwa kuongeza ubunifu ili kwendana na kasi ya teknolojia pamoja na ushindani wa  soko la kibiashara. 

 


Post a Comment

0 Comments