ASILIMIA 95 YA WAKIMBIZI KIGOMA WAGOMA KURUDI NCHINI KWAO

 


Na Mwandishi Wetu, Kasulu.

Asilimia 95 ya Wakimbizi na Waomba hifadhi wa nchi ya  Burundi wanohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu Wilayani Kasulu mkoani  Kigoma, wamegoma kulejea Nchini Mwao,  kwa kile wanachodai bado hali ya amani hailidhishi nakuomba Serikali ya Burundi kuwahakikishia amani ili waungane na wenzao katika kuijenga nchi hiyo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu Siasa Manjenje wakati wa mkutano wa viongozi wa Idara ya wakimbizi kutoka Tanzania na Burundi pamoja na  kamati za ulinzi na usalama walipotembelea  kambini hapo.

Kwa upande wake mkurugenzi idara ya huduma kwa wakimbizi Nchini, Sudi Mwakibasi amewataka wakimbizi kuendelea kulejea kwa kasi na kulingana na Warundi wenzao katika Kujenga taifa lao.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu waziri wa mambo ya ndani nchini Burundi Nibona Bonansize  amewahakikishia wakimbizi hao Nchi ya Burundi kuwa Shwari na kwamba hawana budi kuendelea kuishi kama wakimbizi bali wakajenge Nchi yao.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewaondoa wasiwasi laia hao kutoka nchini Burundi kwa kusema kuwa Jumuiya ya afrika Mashariki, itahakikisha mataifa ya jumuiya hiyo yanakuwa na amani na hivyo wananchi kufanya mwingiliano wa kibiashara na kuondokana na ukimbizi 

Kwa niaba ta wakimbizi Nduwimana Jeradi alisema hadi sasa unashindwa kurejea nchini Burundi kwa sababu hawaamini kama hali ya usalama imeimarika nchini mwao.

 

Post a Comment

0 Comments