CHANGAMOTO ZA MBOLEA ZAWATESA WAKULIMA KIGOMA



Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Wakulima kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Kigoma, wamelazimika kuweka kambi kwa mawakala wa kuuza mbolea ya ruzuku ya serikali, kutokana na kuendelee kusubiri mbolea hiyo kwa zaidi ya wiki moja kwa mawakala wanaosambaza bila mafanikio, huku changamoto ikitajwa kukosekana kwa stika licha ya mbolea hio kufungiwa kwenye maghala ya kuuzia.

 

Wakizungumza na Kituo hiki Wakulima hao wamesema wanalazimika kutumia ghalama kubwa za kulala katika nyumba za wageni ili kusubiria mbolea huku changamoto hio ikikwamisha shughuli za kilimo.

 

Akieleza sababu za kutogawa mbolea kwa wakati, mmoja wa wakala wa kusambaza mbolea ya ruzuku Kutoka kampuni ya ETG Sebastian Raurent amesema changamoto ya sitika ndio imekwamisha ugawaji wa mbolea hiyo, na kwamba juhudi za kuweka sitika zinafanyiwa kazi.

 

Aidha Afisa kilimo, mifugo na uvuvi manispaa ya Kigoma Ujiji Evance Mdee alikanusha changamoto ya ukosefu wa mbolea kuwepo kwa sasa na kuzitaka kampuni zinazosimamia zoezi la ugawaji kulifanikisha kwa wakati.

 


Post a Comment

0 Comments