ONGEZEKO LA WATU LA HATARISHA UHAI WA MISITU NA VYANZO VYA MAJI

 


Na Mwandishi Wetu, Kigoma

ONGEZEKO la watu kutoka mikoa mingine nchini katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, imepelekea wimbi la uvamizi wa misitu na vyanzo vya maji, na kufanya Shughuli za kilimo na ufugaji ambazo zimepeleka uharibifu mkubwa hasa katika mto Malagarasi na ukataji wa misitu maeneo ya Hifadhi.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Hanafi Msabaha akiwa katika mkutano na wananchi wa wilaya hiyo alikiri uwepo wa ongezeko la watu hasa maeneo ya Hifadhi ambao wameathiri shughuli za Uhifadhi wa misitu, na kuharibu vyanzo vya mito kwa kufanya shughuli za kilimo.

“Kwasasa tunakabiliwa na changamoto japo ni changamoto nzuri kama tutaitumia vizuri, changamoto ya ongezeko la watu ambao wamevutiwa kuja kigoma kwa shughuri za ufugaji na kilimo, sasa ongezeko hilo linakuja na changamoto zake ikiwemno uharibifu wa mazingira ya misitu.

“Tuna kazi kubwa viongozi ya kuwaelimisha wananchi namna bora ya kutunza mazingira ili tunufaike na ujio wao badala ya wao kuendelea kuharibu mazingira jambo ambalo ni hatari kwetu” alisema Msabaha.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuendeleza usitawi wa mto Malaharasi ambao unachangia kwa kiwango kikubwa asilimia sabini na tano maji ya ziwa Tanganyika.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliomba elimu kuzidi kutolewa na kwamba wanao fanya shughuli za uvamizi wanatakiwa kuondolewa halaka iwezekanavyo kwa kuwa wanafanya uharibifu unaopelekea madhala ya siku za usoni.

 

Post a Comment

0 Comments