CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KIGOMA CHAAZIMIA KUJIBORESHA ZAIDI

Rais wa umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo akifungua mkutano mkuu maalum kwa wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa Mkoa wa Kigoma(KGPC)


Na Editha Karlo, Kigoma

CHAMA cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma (KGPC) Kimefanya mkutano mkuu maalum, ambao umepitisha maazimio kadhaaa yenye lengo la kuboresha hali ya utendaji kazi kutoka mafanikio yaliyopo sasa na kuwa bora zaidi.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ambaye ni mwenyekiti wa KGPC Deogratis Nsokolo alisema UTPC inakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika kuvijengea uwezo vilabu vya habari nchini ili kuwa na mikakati ya kujiimarisha na kujiendeleza.

“Sasa hivi kila klabu za waandishi nchini zitatakiwa kuwa na miradi ambayo itasaidia kuimarisha club hizo ili hata wafadhili wetu watakaposuasua kutoa ruzuku au kujiondoa basi vilabu viwe na uwezo wa kujiendesha bila kuyumba kupitia miradi yao”alisema.

Nsokolo alisema kuwa sasa hivi UTPC watatoa pesa kwa klabu kulingana na mahitaji yake hivyo ni lazima klabu iombe fedha kwa mahitaji halisi ya klabu yake na bajeti hiyo itapitishwa na UTPC, pia klabu itapewa fedha kulingana na idadi ya wanachama wake.

Katika hatua ya kujiimarisha kwa KGPC, kuna miradi mbalimbali ambayo mkutano mkuu imependekeza na kuwekwa chini ya kamati ya miradi kwa uchambuzi ili hatua za utekelezaji wa miradi hiyo uanze.

Nsokolo alisema Mkurugenzi mkuu wa UTPC Keneth Simbaya amehaidi kutembelea klabu ya Kigoma mwakani ili kujionea shughuli za maendeleo kwenye tasnia ya habari kwenye klabu hiyo.

Nao baadhi ya wanachama wa KGPC wakichangia kuhusu maazimio hayo waliwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa UTPC kwa kuleta maazimio yenye kuzifanya klabu ziwe na misingi imara hasa katika usimamizi wa fedha.

Walisema baadhi ya klabu zimekuwa na migogoro lakini kwenye maazimio ya mkutano mkuu wa UTPC wameweka mwongozo maalum wa utatuzi wa migogoro katika klabu.

“Haya maazimo ni mazuri na ndo maana tumeyapitisha tunachotakiwa ni kuyafanyia kazi kwaajili ya kuimarisha na kuendeleza klabu zetu”alisema mwanachama Prosper Kwigize

Naye katibu Mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoman (KGPC) Mwajabu Hoza aliwasisitiza wanachama wote kulipa ada zao kwa wakati kila mwaka ambayo ni mapato ya msingi na hadi kufikia February 28, 2023 mwanachama yeyote atakaye kuwa na deni atafukuzwa uanachama na hii ni kwa mujibu wa katiba.

 

Post a Comment

0 Comments