RAIS AAGIZA MIL. 960 ZA UHURU ZIJENGE MABWENI



Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Mhungano wa Tanzania Mhe.  Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa fedha zilitengwa kwaajili ya maadhimisho ya sherehe za uhuru mwaka 2022  Tsh. Milioni 960 zipelekwe ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili  zitumike kujengea  mabweni katika shule za msingi 8  za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na utaratibu Mhe. George Simbachawene  leo tarehe  5  Disemba 2022.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Mkoani  Shinyanga, Goeko iliyopo Mkoa wa Tabora,Darajani Mkoani Singida,Mtanda iliyopo Mkoa wa Lindi, Songambele Mkoa wa Manyara,Msanzi iliyopo Mkoni Rukwa, Idofi iliyopo Mkoani Njombe pamoja na shule ya msingi Longido iliyopo katika Mkoa wa Arusha.

Amesema shule hizo zimekwisha ratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na tayari zimekwishagawiwa fedha hizo kwaajili ya kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Hii ni dhamira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenya  mahitaji maalum hapa nchini, hili ni jambo kubwa na lakishujaa na la kupongezwa sana na wananchi wote wa Tanzania” Ameeleza Simbachawene

Post a Comment

0 Comments