SERIKALI YAENDELEA KUPANUA FURSA ZA SOKO LA KOROSHO DUNIANI

 


Na Mwandishi Wetu, Mtwara.

Serikali imesema inaendelea kupanua fursa za soko la korosho Duniani ambapo kwa sasa tayari korosho za Tanzania zikiwemo korosho ambazo tayari zimebanguliwa zimefika katika soko la Marekani na Ulaya.

DC wa Mtwara, Dustan Kyobya kwenye mahojiano maalum amesema “Kuna soko la Marekani zimeshafika, sasa soko la Uholanzi korosho zimefika na tuna mwenye kiwanda ambaye yupo hapa anatoka Uholanzi, kwahiyo tutafungua soko la Ulaya, Marekani na Asia, kwahiyo kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kufanya ubanguaji ni bora zaidi nawaomba Wawekezaji waje wawekeze Mtwara"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho, Domina Mkangara akizungumzia sababu za bei kuwa ndogo msimu huu amesema “Sio Tanzania pekee inazalisha korosho Duniani tuna zaidi ya Nchi 30 zinalisha korosho, ili kupata soko la uhakika tunahimiza Wakulima kufanya ubanguaji badala ya kuuza korosho ghafi zenye maganda”

Aidha Dr. Kapinga kutoka Chuo cha Utafiti wa Kilimo Nariendele amesema “Unaweza kupata juisi na wine kutoka kwenye mabibo (matunda ya korosho), pia korosho inaweza kutengeneza maziwa na siagi"

 

Post a Comment

0 Comments