UJENZI WA KITUO CHA BIASHARA KIBONDO WAFANYABIASHARA WASEMA ITAINUA UCHUMI WAO


Na James Jovin, Kibondo

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Biashara eneo la mpakani mwa Burundi na Tanzania katika Kijiji cha Mkalazi wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma baadhi ya wafanyabiashara wamesema kuwa soko hilo litasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa nchi zote mbili.

Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo Deocres Rutema alisema kuwa tayari serikali imekamilisha miundo mbinu mbali mbali inayohitajika katika kituo hicho cha biashara kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi katika kata ya mabamba  na kilichobaki ni wafanyabiashara  kujitokeza na kuanza kuwekeza katika viwanja vya makazi, maduka, hotel , shughuli za ibada na viwanda vidogo vidogo.

Aidha alisema kuwa eneo hilo la Mpakani katika Kijiji cha Mkalazi wameliandaa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kibiashara na kupunguza mizunguko ya wageni kutoka Burundi wanaoingia nchini kwa lengo la kufanyabiashara na kuongeza kuwa bidhaa zote zilizoruhusiwa zitakuwa zinapatikana katika kituo hicho

Wakiongea katika Kituo hicho kinacholenga kuwakutanisha Raia wa Tanzania na Burundi wakati wa ziara fupi iliyoongozwa na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo baadhi ya wafanyabiashara Fredcdick Mathias na Kahili Bushize walisema kuwa kituo hicho cha biashara kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa wajasiliamali na taifa kwa ujumla.

 

Post a Comment

0 Comments