UNHCR NA MAHAKAMA KUU KANDA YA KIGOMA KUHAKIKISHA VIFAA VYA TEHAMA VINAPATIKANA

 


Na Kadislaus Ezekiel, Kigoma

Shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma imezindua mpango wa pamoja wa kuhakikisha vifaa vya tehama vinapatikana kwa mahakama zote za wilaya kwa lengo la kuwezesha utatuzi wa kesi mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Akizunguza katika hafra ya makabidhaino ya vifaa vya tehama Jaji mfawidhi mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma  Lameck Mlacha alisema upatikanaji wa vifaa hivyo ni hatua mhimu katika kuhalakisha kumaliza mashauri mbalimbali ya jinai.

Alisema licha ya Juhudi Hizo Mahakama za Wilaya ya Buhigwe na Uvinza bado zinakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya Tehama na kwamba juhudi zinahitajika kama hizo kuhakikisha wananchi wanapata huma bora na kwa wakati unaotakiwa.

Kwa upande wake afisa hifadhi mwandamizi shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi mkoa wa Kigoma Peter Muriuki alisema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni baada ya mahakama kuhitaji vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata hduma za kimahakaam kwa njia ya mtandao na kuwapunguzia ghalama za kusafiri kutoka umbali mrefu.

Alisema juhudi hizo pia, zinawalenga wakimbizi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma, ambao watahusika kupata huduma za kimahakama kwa njia ya mtandao wakiwa katika maeneo ya kambi za wakimbini na kuwawezesha kupata haki hiyo kwa wakati.

Aidha baadhi ya wadau wa sheria mkoani Kigoma, walieleza tija zaidi kutokana na upatikanaji wa vifaa vya tehama katika maeneo ya kazi na kwamba hatua hiyo ni kuona wananchi wanapata huduma kwa wakati na kuwaondolea usumbufu ikiwemo kutumia ghalama kubwa za usafiri.

Post a Comment

0 Comments