CHANGAMOTO ZA ELIMU ZAITESA MIKOA 9 YA TANZANIA


Na Kadislaus Ezekiel, Kigoma

Mikoa Tisa ya Tanzania Bara imebainika kuwa na changamoto ya upungufu wa Walimu na mwamko duni wa wazazi katika masuaal ya elimu jambo linalopelekea kuwa na ufaulu hafifu wa matokeo ya darasa la saba pamoja na watoto wa kike kuolewa mapema na kushidwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Hayo yameelezwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa Shule Bora ambapo pia mafunzo yalitolewa kwa wandishi wa habari ishirini, Wakurugenzi wa Radio na Maafisa Habari kutoka Halmashauri za mkoa wa Kigoma, wenye lengo la kuhamaisha elimu bora, Jumuishi, endelevu na kuhakikisha usalama unapatikana kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Mradi huo unatekelezwa na Serikali Chini ya Wizara ya Habari na TAMISEMI kwa udhamini wa shirika la Msaada la Uingereza UKaid ambao utagusa mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Rukwa, Katavi, Pwani, Tanga, Simiyu, Mara, Singida na Dodoma.

Akizungumzia baadhi ya Changamoto za Jumla zinazokwamisha elimu Bora, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Kigoma David Mwamalasi amesema ni pamoja na vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu na ufaulu duni.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Celestine Bukango amesema mradi utajikita katika maeneo makuu manne ya ufundishaji, ujifunzaji na kuimarisha mifumo ya utoaji wa habari na takwimu kwa usahihi huku Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Paulina Ndigeza ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa, amesema mradi huo unalenga kuleta mabadiliko katika elimu Msingi na kukuza ufaulu.

Mradi wa Shule Bora unatarajia kutumia pauni za uingereza milioni 89 sawa na bilioni 271 za Kitanzania ambao utatekelezwa hadi mwaka 2027.


Post a Comment

0 Comments