HOSPITALI YA WILAYA RORYA YATELEKEZWA, NAIBU WAZIRI DUGANGE ATOA MAELEKEZO YA KUIFUFUA

Na Mwandishi Wetu, Rorya
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya kusimamia ukamilishaji wa Majengo muhimu ya awali katika Hospitali ya Wilaya Rorya  kabla ya tarehe 28 Februari 2023 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Ametoa maelekezo hayo Januari 15, 2023 wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya Rorya na kukuta majengo saba ya awali yaliyojengwa tangu 2018 yakiwa yametelekezwa na hakuna Mkakati wowote wa kuyakamilisha.

“Menejimenti ya wilaya mkae muweke mpango mkakati wa kukamilisha majengo muhimu ya awali ambayo ni Jengo la mama na Mtoto, wodi ya wazazi, Jengo la upasuaji na Maabara yanakamilika ifikapo tarehe 28 Februari 2023”

Dkt. Dugange amesema Serikali iliteta shilingi bilioni moja na milioni 500 tangu mwaka 2018 kujenga Majengo saba ya awali lakini fedha hiyo ilikosa usimamizi na mpaka sasa imepita miaka mitano majengo hayajakamilishwa na yametelekezwa.

Aidha, Dkt. Dugange ameelekeza Jengo la kufulia, Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la  Upasuaji kwa wananume na wanawake na yenyewe yakamilishwe kabla ya tarehe 30 April, 2023 na kuanza kutumwika.

Ameagiza uchunguzi kwa Watumishi waliosimamishwa ambao ni Afisa manunuzi na Mhandisi wa Wilaya kwa tuhuma ya uzembe na ubadhilifu uliotokea katika Hospitali hiyo ukamike mapema wakikutwa na hatia wachukuliwe hatua za kisheria.

Pia, Dkt. Dugange amekemea tabia ya Watumishi wa Halmashauri hiyo kuongeza gharama za miradi kwa manufaa yao binafsi na kulalamika kuwa fedha hazitoshi hata kabla ya kuanza utekelezaji  wakati Miradi kama hiyo inatekelezwa katika Halmashauri nyingine nchini na inakamilika.

Post a Comment

0 Comments