MRADI WA MAJI MANISAPAA YA KIGOMA UJIJI WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 92


Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Mamla ya maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA imesema kuwa mradi wa maji wa Amani Beach ambao umefikia asilimia 92 unatarajia kuwa suluhisho la upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

Hayo yanabainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Jones Mbike wakati Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ilipotembelea Manispaa ya kigoma ujiji ilipotembekea chanzo cha mradi huo.

Kwa upande wake Katibu wa siasa na uenezi Manispaa ya Kigoma Haruni kambiro anawapongeza kuwasa kwa kazi nzuri inayoendelea ya ujenzi wa kitekeo kipya cha maji katika mradi wa chanzo cha maji cha amani beach.

Nao baadhi ya madiwani katika halmashauri ya kigoma wanapongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita kwa kuamua kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwani wananchi walipoteza muda mwingi katika utafutaji wa maji.

Post a Comment

0 Comments