MTOTO ACHOMWA MOTO VIGANJANI NA MAMA YAKE

Na James Jovin, Kibondo.
Mtoto mwenye umri wa miaka sita mkazi wa mtaa wa Kanyamahela wilayani Kibondo mkoani Kigoma amefanyiwa ukatili na mama yake wa kambo kwa kuunguzwa viganjani na mkaa akituhumiwa kudokoa mboga.

Tukio hilo lilitokea zaidi ya wiki moja iliyopita lakini limegunduliwa jana jumatatuJanuary 16, 2023 ambapo majirani walimuona mtoto huyo akiwa mdhaifu na hawezi kucheza na wenzake, hata hivyo ilichukua muda mtoto huyo kusema kilichotokea kwa kuwa alikuwa amekatazwa na mama yake kusema.

Akizungumuza akiwa chini ya ulinzi wa viongozi wa mtaa wa Kanyamahela mama wa kambo wa mtoto huyo bi. Evelina Jackob amekili kufanya tukio hilo na kwamba alishikwa na hasira kali kutokana na mtoto huyo kuwa na tabia ya kudokoa chakula mara kwa mara.

Kwa upande wake baba wa mtoto huyo bw. Antony Nestori amesema kuwa hata yeye hakuwa na taarifa za kuungua kwa mtoto huyo licha ya kuishi nae nyumba moja na kwamba ilifahamika wakati akiwa shuleni baada ya kushindwa kuandika kwani bado anasoma elimu ya awali.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa katerela wamesema kuwa swala hilo ni ukatili kwa watoto wadogo na halipaswi kufumbiwa macho na kwamba mtoto ni wa serikali licha ya kwamba kumtunza ni wajibu wa mzazi husika

Aidha mwenyekiti wa tawi la Katerela bi. Herena Misigaro amesema kuwa taarifa za kuungua kwa mtoto huo zilipatikana kwa majirani ambao waliona kuwa tukio hilo si la kawaida na ndipo ufuatiliaji ukafanyika ili kubaini chanzo cha tukio hilo

Baada ya mahojiano na viongozi wa mtaa wa Katerela kwa kushirikiana na wananchi viongozi wamechukua maamuzi ya kupeleka swala hilo ofisi za ustawi wa jamii wilaya ya Kibondo kwa ajili ya mahojiano zaidi na maelekezo ya kinidhamu.

Post a Comment

0 Comments