ONGEZEKO LA WATU CHANZO CHA UKUAJI WA MIJI NA VIJIJI TANZANIA.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi imesemaTanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na kasi kubwa ya ukuaji wa miji na vijiji kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu linalosababisha kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi yaliyopangwa na yenye usimamizi mzuri na salama.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Mh Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa Kitaifa wa wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa miliki za Ardhi (LTIP) ikiwa ni Mradi wa kwanza kwa ukubwa katika sekta ya ardhi kuwezeshwa na Benki ya Dunia Kusini kwa nchi za chini ya Jangwa la Sahara ambapo mradi huu utatumiwa na Benki ya Dunia kupima uwezo wa watanzania kusimamia na kutekeleza miradi mikubwa katika Sekta ya Ardhi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akitoa Taarifa ya Mradi wa uboreshaji usalama wa Miliki za Ardhi(LTIP) katibu mkuu wa wizara ya Ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi Allan Kijazi amesema mradi huo ulisainiwa na Benki ya dunia Tarehe 21 january mwaka 2022 ambapo jumla ya Fedha Billion 346 ziliidhinishwa kwa kusaini mkataba wa pamoja kati ya Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania kwa lengo la kutekeleza usalama wa Miliki za Ardhi nchini.

Kwa upande wao badhi ya wakuu wa mikoa waliohudhuria mkutano huo akiwemo  mkuu wa mkoa Tanga Omary mgumba alikuwa na haya ya kusema.

Mradi umepangwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano (5) kuanzia Mwezi Julai, 2022 hadi mwezi Juni,2027 katika Mikoa 16 ya Pwani,Simiyu,Iringa,Tanga,Tabora, Geita,Kigoma,Mara,Shinyanga,Dodoma, Mbeya,Kilimanjaro,Ruvuma,Songwe, 
Katavi na hivi na Mkoa wa Arusha zenye jumla Ya Halmashauri 41.

Post a Comment

0 Comments