RAIS UTPC AMPONGEZA WAZIRI NAPE MNAUYE


Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Rais wa Umoja wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratus Nsokolo amempongeza Waziri wa Habari nchini Mh Nape Mnauye kwakuunda kamati itakayokuwa na kazi ya kuchunguza haki ya uchumi katika vyombo vya habari nchini.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Rais Nsokolo ameandika hivi:

"Hongera sana Mheshimiwa waziri wa habari nchini Mh. Nape Mnauye kwa kuunda kamati hii, hii ni hatua nyingine tunashuhudia Serikali ikitekeleza azma yake ya kutatua changamoto ya sekta ya habari nchini kwa vitendo.

Pamoja na mambo mengine Kamati hii inakwenda kuangalia utaratibu wa( ajiira) mikataba ya waandishi na hali ya kiuchumi katika vyombo vya habari na kutoa maoni na mapendekezo, waandishi wa habari wanasubiri kwa hamu report ya kamati baada ya miezi mitatu.

Nawapongeza nyote Mlioteuliwa mkiongozwa na Mwenyekiti Tido Mhando. Kwa namna ya pekee nampongeza Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya kwa kuwa mmoja wa wajumbe katika kamati hii muhimu.

Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini (Union of Tanzania Press Clubs-UTPC) tutatoa ushirikiano kwa kamati katika press clubs zote nchini na kwa waandishi wote, nawatakia kazi njema.

Deogratius Nsokolo
President -Union of Tanzania Press Clubs -UTPC."

Post a Comment

0 Comments