TAASISI ZA WIZARA YA FEDHA ZAHIMIZWA KUWASILIANA KIMKAKATI

Ma Mwandishi Wetu, Morogoro
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wametakiwa kuwasiliana kimkakati ili kufikisha taarifa zinazohusiana na Wizara pamoja na Taasisi zake kwa wananchi kwa kuzingatia viwango na kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu (sehemu ya rasilimali watu), Bw. Benjamini Chilumba, katika ufunguzi wa kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, lililofanyika mkoani Morogoro.

Alisema kuwa ushiriki katika kongamano hilo ni ishara njema kwa ustawi wa Wizara na Taasisi zake katika kukuza na kuimarisha Mawasiliano kwa Umma na kuwa michango, ushauri na mapendekezo yatakayotolewa kupitia majadiliano yatafanyiwa kazi ili kuboresha zaidi Kongamano lijalo pamoja na kuendeleza mahusiano mazuri ya kimawasiliano kati ya Wizara na Taasisi zake.

‘‘Ninawaagiza Wakuu wa vitengo vya mawasiliano wote kuendelea kutumia jukwaa hili kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau wetu, ni matumaini yangu kuwa siku za usoni kongamano hili litakuwa ni miongoni mwa makongamano bora na makubwa zaidi nchini’’, alisema Bw. Chilumba.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia sekta ya mawasiliano imebadilika hivyo kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kujadili, kujenga ukaribu na kukumbushana mambo muhimu ya mawasiliano na wadau ndani na nje ya taasisi za wizara.

Kongamano lilihudhuriwa na wakuu wa vitengo vya mawasiliano vya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikiwemo, @gpsatanzania , @self_mf , @psptbofficial, @institute_of_rural_development, @tratanzania @ofisi_ya_msajili_wa_hazina @ifm_updates @tia_tanzania @iaa_tz @utt.amis @nbaatanzania, Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA), Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) na Hazina Saccoss.

Post a Comment

0 Comments