TATHMINI VYANZO VYA MAPATO KUWEZESHA HALMASHAURI NCHINI KUJITEGEMEA


Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
MKURUGENZI wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI John Mihayo Cheyo amesema ofisi yake inafanya zoezi la tathimini ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashuri zote 184 Tanzania Bara.

Amesema zoezi hilo limeanza Januari 9 mwaka huu na linafanyika kwenye Halmashauri na mikoa yote mchini na kwamba linajumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,Wizara ya Fedha,Ofisi ya Mkoa husika na Halmashauri zake.

Akizungumza katika mahojiano maalum Mkoani Ruvuma,Mkurugenzi huyo wa Sera na Mipango amesema kwa ujumla wakurugenzi wa Halmashauri nchini kote wamefurahia zoezi la tathimini  ya ukusanyaji wa mapato na wameshauri liwe zoezi endelevu.

“Zoezi hili la tathimini ya ukusanyaji mapato ambalo linafanyika nchi nzima linaweza kutuongezea mapato mengi kwenye Halmashauri na hatimaye kuzifanya Halmashauri zetu kuanza kujitegemea’’, alisisitiza Cheyo.

Hata hivyo amesema kukamilika kwa zoezi hilo kutawezesha kufanya makisio ya mapato kwa uhalisia katika Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Mkurugenzi huyo anawapongeza  viongozi wote wa TAMISEMI,Kamishina Mkuu wa TRA na makatibu tawala wa mikoa yote nchini kwa kusimamia kikamilifu zoezi la tathimini ya ukusanyaji mapato.

Kwa upande wake Mchumi Ofisi ya Rais TAMISEMI Flugence Matemele  ambaye alikuwa kiongozi wa Timu ya  Tathimini ya kusanyaji mapato ya ndani kwenye Halmashauri  za mkoa wa Ruvuma,amesema zoezi limekwenda vizuri na wakurugenzi wa Halmashauri wametoa ushirikiano wa kutosha.

Amesema katika tathimini hiyo wamefanikiwa kuchambua chanzo cha mapato kimoja kimoja kwa kila Halmashauri kuanzia vyanzo vikubwa wanavyojitegemea  ambavyo vimebainika vinachangia mapato kuanzia asilimia 22 hadi 58.

Matemele amesema wakati wanafanya uchambuzi huo wamebaini kuna uwekezekano mkubwa wa vyanzo hivyo vya mapato kukusanya mapato mengi zaidi kama vitasimamiwa kwa nguvu zaidi.

“Wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wao wamethibitisha bado walikuwa wanafanya makisio ya bajeti ya kukusanya vyanzo vya mapato kwa kutumia uzoefu tu,lakini katika tathimini hii

Post a Comment

0 Comments