WADAU WAJITOKEZA KUTAKA USHIRIKIANO ELIMU YA UFUNDI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Shirika lisilo la kiserikali la Global Faith Partner linalopambana na umaskini kupitia elimu ya ufundi stadi.

Timu hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Michael Vallez ilimtembelea Waziri Mkenda jijini Dodoma Januari 18, 2023 ili kujitambulisha na kujadili fursa za ushirikino na baadhi ya vyuo vya ufundi nchini.

Katika mazungumzo hayo Waziri Mkenda amesema kupitia ushirikiano na shirika hilo utawezesha wanafunzi na wakufunzi wa vyuo vya ufundi nchini kupata uzoefu wa kimataifa.


Post a Comment

0 Comments