WANAFUNZI 2,096 WALIOFAULU MTIHANI WA MARUDIO WAPANGINA SHULE

Na Mwandishi Wetu, 
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Kamati za uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza imewapangia shule wanafunzi 2,096 waliokuwa na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza 2023.

Wanafunzi hao ni kati ya wanafunzi 2,180 wakiwemo wavulana 1,112 na wasichana 1,068 sawa na asilimia 99.36 ya waliofanya mtihani wa marudio Desemba 21-23, 2022.

Baraza la Mitihani la Tanzania lilitoa fursa ya wanafunzi 2,194 wakiwemo wavulana 1,117 na wasichana 1,077 kurudia mtihani huo baada ya matokeo yao kufutwa kwa mujibu wa kifungu 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani 2016 kikisomwa pamoja na kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha sheria cha Baraza la Mitihani Sura ya 107.

Taarifa iliyotolewa Januari 15, 2023 na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe imebainisha kuwa taratibu za kuwapangia shule wanafunzi hao zimekamilika na wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizopangiwa kuanzia tarehe 15.01.2023.

“Ofisi ya Rais-TAMISEMI imepokea matokeo ya mtihani huo ambapo jumla ya wanafunzi 2,096 wakiwemo wavulana ni 1,073 na wasichana ni 1,023 sawa na asilimia 96.15 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamepata sifa ya kuchaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika Shule za Sekondari za Serikali.”

“ Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Kamati za Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika mikoa husika imekamilisha zoezi la kuwapangia shule wanafunzi wote 2,096 katika Shule mbalimbali za Sekondari.”

Amesema maandalizi ya kuwapokea wanafunzi hao yamekamilika na wanataarifiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kuanzia Jumatatu Januari 16, 2023 ili kuanza masomo.

“Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.”

“ Pia mwanafunzi, Mzazi/Mlezi atakayekuwa na suala linalohitaji maelekezo au ufafanuzi zaidi aende katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri au apige simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210

Post a Comment

0 Comments