WANAFUNZI ZAIDI YA 27,000 HAWAJARIPOTI KIDATO CHA KWANZA, WAZIRI KAIRUKI AWAJIA JUU

Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amekerwa na hali ya asilimia 55.2 ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Tanga kutoripoti shule.

Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo mkoani Tanga Tar 16.01.2023 wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za  Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi  na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri  kwenye kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika shule ya sekondari Tanga ufundi.

Amesema takwimu za wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza si ya kuridhisha katika mkoa huo.

“Ukiangalia kwenye elimu ya awali mpaka sasa uandikishwaji ni asilimia 82 , lakini nilitamani nisikie kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ni asilimia ngapi ili nao tusiwaache nyuma.”

“Kwa upande wa uwandikishwaji wanafunzi darasa la kwanza mmefikia asilimia 87.7 lakini changamoto inakuja kwenye kuripoti wanafunzi wa kidato cha kwanza.”

Amesema mpaka Januari 13, mwaka huu zaidi ya wanafunzi 27,867 ambao ni sawa na asilimia 55,2 hawajaripoti shule huku walioripoti kwa Wilaya ya Kilindi ni asilimia 11 pekee.

Mhe. Kairuki amesema mpaka sasa ni asilimia 44.8 pekee ya wanafunzi ndio wameripoti shule katika mkoa huo na kusisitiza kuwa ni lazima kila kiongozi kuhakikisha takwimu hizo zinabadilika ndani ya muda mfupi.

Amesema kati ya wanafunzi 27,867 ambao hawajaripoti shule, asilimia kubwa imechangiwa na Wilaya ya Kilindi ambayo ni asilimia 11 pekee ndio walioripoti huku Korogwe Mji ikiwa ni asilimia 22.78,  Korogwe TC asilimia 30.21, Handeni TC asilimia 42.55, Handen DC asilimia 45.86, Bumbuli asilimia 53.26, Mkinga asilimia 27.98 Muhenza asilimia 50 Pangani 52 na Tanga jiji 76.23

“ Je hii ni sawa jamani? Hivyo kila mmoja kwa kadri inavyowezekana takwimu hizi zibadilike ndani ya muda mfupi sana. Haiwezekani tupo siku 16 ya mwezi wa kwanza na watoto zaidi ya 27,867 hawajaingia shule. “

Post a Comment

0 Comments